Mjue Chuma Ulete wa Biashara yako

Chuma ulete ipo tena sana tu, na kuendesha biashara bila kuweka kumbukumbu pia kupo. Chuma ulete ndio kiboko.
 
We jamaa hujui lolote kwenye biashara zaidi ya kuuza maneno tu,unaongelea mabenki sijui makampuni,wakati chuma ulete wanakaba kwenye biashara za mtaani,nenda yombo dovya kafungue duka la rejareja uone mziki wake,usipojipanga utalizwa...binafsi njia ya kukabiliana na hawa watu ni kuweka bible kwenye droo la hela za mauzo hapo unapeta tu hata waje chuma ulete 100 hawafui dafu
 
Ulivotoa mfano wa mabenki tuu nmekuouuza. Yaan hauna ujifunzalo. Ukitaka kuhakikisha kafanye biashara. Utagundua.

Ndugu yangu lisemwalo lipo watu hawawezi kujitungia tuu uwongo kwa maslah ya naani kwanza??
 
Mimi nimetoa mtazamo na kile nnachokijua kuhusu biashara. kama na ww wajua zaidi ya hapo nipe elimu hasa kuhusu huyo mzee Sadick.
Chuma ulete ipo na yupo karudie huo utafiti wako Mkuu!
 
Utakua wewe ndie Mkuu wa Chuma ulete so unatetea... Bank ndipo kuna chuma ulete za kufa mtu kawaulize wale maTeller huwa wanalia kila siku na wengi walishindwa kulipa majazio ya hasabu za siku wamefukuzwa makazini bila kujilinda kazi ya u Teller ni hatari mno... Nenda Bank yeyete kawaulize Mateller kuhusu Chuma ulete and then lete thread nyingine humu JF.

Kuna chuma ulete wa mitaani wao huomba coin za mia mia ogopa sana hao
 
Aisee kumbe mateller wanaisoma
 
Usaiache hela kwenye draw/kibox zaidi ya chenji ndogo ndogo
 
Una point nzuri sana ila kuna ukweli ulio wa kina sana unapaswa kuujua nikipata nafasi nitaeleza
 
Leo nakili kabisa chuma ulete ipo tena ipo nimetoka kupigwa pesa zangu sasa hv yaani sikuwa nikiamini aya mambo kabsa lakini Leo kilicho nitokea nakubali chuma ulete noma...
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza, hiyo mada ni mtazamo wako wa kishule shule ila kiuhalisia umepotoka.sumaku za kijadi zipo yaani hii sayansi ni ya kipekee.
Usiongee kama haujawahi kukutana nayo.
Mtaani wapo kibao haswa wale wa elfu kumi kwa kitu cha mia tatu au kuomba chenji
 
Leo nakili kabisa chuma ulete ipo tena ipo nimetoka kupigwa pesa zangu sasa hv yaani sikuwa nikiamini aya mambo kabsa lakini Leo kilicho nitokea nakubali chuma ulete noma...
Peleleza vzuri, kuna mtu ana access na unapotunzia pesa amejichukulia
 
kijitu kimeajiriwa uko,kimezoea kujadili madaraja na nyongeza afu leo kinafundsha wafanyabiashara eti hakuna chuma ulete,pumbaaavu(in ray kigosi voice),,ingia mtaani uanZishe biashara uone,,hafu siku hizi hadi bodaboda wana chuma ulete,,akikupa chenchi ujue inarudi kwake,,huku kuna watu wana madude ya naijeria wanaingiza hadi millioni kwa siku,,,wew rizika na tgts zako,kuchomekea na kuwahi asubuhi kazini,,lakini sio kujifanya kuzungumzia chuma ulete kua haipo wakati ata biashara hufanyi... N:B..mimi kama mimi nshabutuliwa M3..nlishtuka kumekucha...hapo nikakubali kujifunza madarasa ya mtaani...wachaa kabisa nakwambia usiombe yakukute
 
Acha kuongopa mkuu Yani chuma ulete wakakupiga m3 hivihivi lete ufafanuzi....???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…