Mbavu mbili
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 1,457
- 874
Hatuwezi kufanya mambo yote wa wakati mmoja nadhani nia ya serikali ni mjema tu baada ya hapo tuhamie kwenye shule za ufundi sasa.
Hivi kumbe ufundi unahitaji watu waliofeli? nilidhani ufundi unahitaji watu wenye uelewa mzuri wa masomo ya sayansi na hesabu, hii dhana ya kuwa kila anayefeli apelekwe kwenye ufundi ndiyo inachangia sekta hii kutokua au kuwa na mafundi vihiyo katika nchi hii. Ufundi ni taaluma inayohitaji watu makini,
Kwangu hii ni thread bora kwa siku ya leo.
sidhani kama umetafakari kwa kina, unataka kutuambia wanaofeli kidato cha 2 na 4 ndo wanasifa za kua mafundi. Yaani mafundi ni watu waliofeli shule.Wakuu
Nimetafakari sana wazo la kuanzishwa shule za Kata na kubaini kuwa lilikuwa zuri, licha ya changamoto za hapa na pale. Ni dhahiri tangu kuanza kwake zimesaidia Watanzania baadhi kutimiza ndoto zao za kielimu.
Ukichunguza shule hizi zimejengwa walau karibu kila kata kuanzia mijini hadi vijijini. Pia kumekuwa na idadi ya wanafunzi wengi wanaofeli mitihani ya kidato cha NNE ukilinganisha na idadi ya ufaulu wao.
Wazo langu:
Tubadili baadhi ya shule za Kata ziwe shule za Ufundi. Wanafunzi watakaofeli kidato cha PILI na cha NNE wahamishiwe katika shule hizo Mpya za ufundi. Huko masomo mbalimbali ya ufundi yafundishwe kwa miaka mitatu au miwili.
Ninafikiri hili litasidia sana kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini mwetu. Pia litaongeza uwezo wa vijana kujitegemea wao wenyewe pindi wamalizapo masomo yao, na Mwisho itapunguza athari mbaya za makundi ya vijana wanaomaliza kidato cha NNE na kupata alama zisizokuwa na msaada wowote katika maisha husika.
Imani yangu ni kuwa si kila mtoto anayefeli masomo darasani basi hana uwezo wa kujifunza masuala mengine katika maisha. Hili litaongeza idadi na chachu ya vijana wasio tegemezi .
Ni imani yangu Shule hizi zikitumika vizuri zitalikomboa taiifa katila masuala mbalimbali.
Naomba kuwasilisha.
sidhani kama umetafakari kwa kina, unataka kutuambia wanaofeli kidato cha 2 na 4 ndo wanasifa za kua mafundi. Yaani mafundi ni watu waliofeli shule.
Nadhani hili ni wazo bora kabisa. Lakini je lina mashiko?? Unajua unaposema kubadili baadhi ya shule za kata kuwa shule za ufundi stadi ,unatakiwa uweke akili mambo kama;
1. Walimu wa shule husika kuhamishwa kupelekwa shule nyingine,~kuna balaa hapo
2. Kuongeza facilities za ufundi ili kukidhi haja~ shida nyingine kwa serikali yetu
3. Je wanafunzi hao waliofeli wengi tayari wana nyimbo 500 za ubongo fleva na script za bongo movie wako tayari kujifunza useremala~ kuwa kama Yusuph baba ake na Yesu? Au umakenika~ kuchezea oil??
all in all this is the splendid and magnificent proposal.
sidhani kama umetafakari kwa kina, unataka kutuambia wanaofeli kidato cha 2 na 4 ndo wanasifa za kua mafundi. Yaani mafundi ni watu waliofeli shule.
Hivi kumbe ufundi unahitaji watu waliofeli? nilidhani ufundi unahitaji watu wenye uelewa mzuri wa masomo ya sayansi na hesabu, hii dhana ya kuwa kila anayefeli apelekwe kwenye ufundi ndiyo inachangia sekta hii kutokua au kuwa na mafundi vihiyo katika nchi hii. Ufundi ni taaluma inayohitaji watu makini,
unacomplecate sana mkuu, kutengeneza furniture kweli kunahitaji watu makin kiasi kwamba mwenye division 4 anakuwa haqualify? tukiwa na vyuo vingi vya ufundi nadhani hatutategemea sana bidhaa za nje, na vijana wengi watajiajiri.