Habari za asubuhi wana jamvi, nimepatwa na mshtuko katika siku za hivi karibuni kuhusiana na mienendo ya makampuni ya simu za mkononi. Huko nyuma ilikuwa ukiingiza vocha pasipo kujiunga na kifurushi au ukabakiza kiasi baada ya kujiunga, baada ya muda mfupi utakuta salio lililobaki limeisha pasipo kujua limetumikaje.
Ukiwauliza wahusika watakuambia eti kama simu yako ina access na internet basi kuna message zinajituma automatically hadi salio linaisha. Siku moja niliacha salio la shs 5,000/= nikisema ningejiunga baadaye, nilivyokuja kutahamaki salio lilikuwa tayari limeondoka.
Na ukiwauliza TCRA wanakushauri uwasiliane na kampuni husika ikishindikana uwasiliane nao kwa barua hadi kufikishana kwenye vyombo vya sheria alimradi unakuwa mlolongo mrefu wa ufuatiliaji na usumbufu mtupu.
Sasa hivi situation imekuwa mbaya zaidi, hata ukijiunga na kifurushi ukiongea kidogo au ukikaa pasipo kuongea utakuta kifurushi kimeisha kabla ya muda wake.
Yaani kama ni ya 24 hrs kifurushi kinaisha kabla ya muda huo kufika. Ninawauliza wanajamvi wenzangu na nyinyi tatizo hili mnalipata. Na kama lipo nini hasa chanzo chake.
Na TCRA wanaemaje maana hatujatangaziwa kama tariff zimepanda.