Mitandao ya Simu za Mikononi, Mmetekwa?!!!!

GalileiGalileo

Senior Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
165
Reaction score
225
Nikiwa mmoja wa Wadau na Watumiaji wa huduma za Mitandao ya Simu za Mikononi haswa upande wa DATA, ninasikitishwa na HUDUMA MBAYA au zilizo CHINI YA KIWANGO nnazopata kwa sasa nikilinganisha na miaka iliyopita. Inasikitisha kuona tunapiga hatua kurudi nyuma badala ya kwenda mbele!

Mimi ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Vodacom zaidi ya miaka 9 sasa, nimekuwa nikitumia internet ya kampuni hii kujifunza, kuhudhuria madarasa ya mitandaoni (online learning), kupata taarifa mbalimbali, kutafuta ujuzi katika kuboresha ufanisi ofisini, kufanya mawasiliano mbalimbali Duniani kwa mahitaji mbalimbali, nk. Nilifika wakati ambapo nilikuwa na-refresh mind kwa kuangalia SERIES mbalimbali mitandaoni moja kwa moja (live) kama vile naangalia TV! Bila kumung'unya maneno, hapa ndipo Dunia ilipo kwa sasa.

Cha kusikitisha, kwa siku za hivi karibuni, nimeshuhudia huduma hii muhimu kwa Dunia ya sasa ikiporomoka kwa mwendokasi ambao haulezeki na hivyo kutuacha sisi Wabongo katika Dunia tofauti na hii walio wenzetu. What's going on here?!!!!
Mwanzo nilidhani ni Voda tu, ila kwa UTAFITI mdogo niliofanya nimegundua kuwa ni MAKAMPUNI YOTE ya simu za mkononi (Mobile Phone Companies), kwani wakati nalalama kuwa sipati huduma niliyozoea toka Vodacom, kwa mshangao nilisikia toka kwa watumiaji wa mitandao mingine kuwa hali ni hiyo hiyo, hata Halotel ambayo imezaliwa hivi karibuni! No way! There must be some common problem somewhere!

Nasubiri kwa hamu toka kwa Wamiliki wa Makampuni haya kujua kama kuna some tangible issues why these services have gone down to this extent!

Ahsanteni na nasubiri majibu, kama na ninyi mmetekwa mseme! Otherwise wajitokeze watumiaji wa mitandao mingine wanipinge kwa evidence kuwa tatizo ni kwa Voda tu au ni kwenye line yangu tu!

NB:
Sijawahi kutumia mtandao wa TTCL kwa kuwa naishi eneo ambalo hawana hiyo huduma ya "mobile", be it voice or data.
 
Natumia Voda hawajawahi kuniangusha kwenye internet ila hawa wanaojiita airtel laini yao nilishatupaga kwasababu speed yao ni afadhali ya kobe
 
Natumia Voda hawajawahi kuniangusha kwenye internet ila hawa wanaojiita airtel laini yao nilishatupaga kwasababu speed yao ni afadhali ya kobe
Unaandika toka pande zipi mdau? Labda nihamie huko! But, ni jana tu nilikuwa nawasiliana na jamaa zangu wa Dar kupitia VOICE communication na huduma ikawa offal! Haya, we mwenzetu uko wapi? Nishtue basi!
 
Unaandika toka pande zipi mdau? Labda nihamie huko! But, ni jana tu nilikuwa nawasiliana na jamaa zangu wa Dar kupitia VOICE communication na huduma ikawa offal! Haya, we mwenzetu uko wapi? Nishtue basi!
Kaskazini mwa nchi mkuu, kwa Gambo
 
Naomba kufafanua zaidi, nimesema kuwa huduma za hii Mitandao ya Simu za Mkononi imekuwa mbaya sana hapa nilipo (Lake Zone) except TTCL ambayo sina ACCESS nayo, na nikakazia kuwa tatizo ni kubwa zaidi kwenye huduma za DATA. Lakini pia hata ukipiga simu au kupokea simu iliyopigwa toka popote probability ya kuongea smoothly kama ilivyokuwa hapo awali ni ngumu sana! Likewise, kwenye SMS, siku hizi ni kawaida kuandika na kutuma SMS halafu ukaona meseji ya "sending......." halafu mwisho ika-fail as if huna bundle! Sijui kama mna-feel hiki nnachokumbuna nacho na ndo maana nikasema someone can prove me wrong with evidence na sio kupitia MIHEMKO ya kijinga, am suffering men!
 
Voda wezi tu, haiwezekani niweke vocha ya Tsh 1000 nijiunge 500 ibaki 500 baadaye nataka kujiunga mia 5 iliyobakia naambiwa kua sina salio, nikawapigia huwenda kunahuduma yoyote nimejiunga pasipokujua nikajibiwa Hakuna huduma yoyote niliyojiunga nayo kuuliza pesa yangu imepoteaje naambiwa nipige baada ya lisaa Kupita..... Kuwapigia tena naambiwa sistimu haionyeshi hivyo hawawezi kuniambia chochote.

Hawa Jamaa O kabisa.
 
Hivi ni kweli hakuna wanaokumbana na changamoto za kuudhi kwenye hii mitandao ya simu za mkononi kama vile kukatikakatika kwa mawasiliano wakati wa kuongea, kutuma sms zikafeli wakati una bundle na kujiunga na data bundle, say ya saa 24 na bundle ku-expire kabla hujafanya chochote cha msingi kupitia bundle hilo?!!!!!
 
Umesema kweli mkuu yaani kama AIRTEL ndio kabisaaa chenga
 
Tupo mkuu
 
Mtandao BORA ni TTCL hii mingine imeshuka sana katika utoaji huduma, nilianza achana na airtel, nikaachana na tigo juzi nimevunja line ya voda

Kwasasa natumia kitu TTCL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…