Umeleta hoja ya msingi sana kwa maana ni wachache sana kati yetu wanaoliangalia hili swala kwa uzito wake.
Ukitoka Dar es Salaam kwa barabara kuelekea Arusha, Mwanza, Kagera, Mbeya, Mtwara, Songea nk unakutana na magunia ya mkaa yanayouzwa kandoni mwa barabara kila sehemu. Hiyo ni mbali na shehena zinazotoka maeneo ya ndani ya misitu husika ambapo maloli huingia kupakia ili kuyafikisha kwa watumiaji. Sehemu nyingine zinaonekana wazi kabisa kuwa miti karibia yote imekatwa na hakuna upandaji mpya!
Swali la msingi lilikuwa ni kama serikali ingeliamua kuweka subsides kwenye gesi ya matumizi ya majumbani gharama yake isingelingana na hasara ya misitu inayopotea.