Kusema ukweli Mimi ni rijali na vigezo vifuatavyo vinathibitisha Hilo.
Nina six pack
Mrefu
Mweusi
Katili kidogo
Sijawahi kupigwa kwenye ngumi.
Nk
Ila udhaifu wangu ukitaka nilie kama mtoto mdogo nirushie dudu washawasha lenye manyoya na likitembea linajinyonga nyonga.
Uoga wangu wa pili ni kuangalia chini ninapokuwa juu gorofani au kupita kwenye madaraja ya kiteputepu (wenyeji wa tukuyu wanayajua) aisee siwezi kabisa miguu inatetemeka na mwili kukaa jasho.
Ila ukiniambia nilale makaburini au nitembee makaburini usiku siogopi.
Kimsingi kila mwanaume ana uoga wake kuna jamaa yangu akimuona paka anajificha nyuma yangu ila nimbabe.