Mijira imekatwa

Viongozi hawa wa Kiafrika wanaoua na kutesa? wasiotaka kuona mtu mwenye mitazo au mawazo tofauti?
Viongozi hawa ambao ukiwaambia ukweli wanakimbilia kusema umetumwa na mabeberu? Viongozi wa Kiafrika ni wakoloni wenye roho mbaya zaidi ya wakoloni Wazungu, advantage yao na kinachowaponza wale wenye upeo mdogo wa kuchanganua mambo ni pale wanapojiona wanafanana rangi na hao wakoloni wa Kiafrika.
Watu kwa upeo mdogo wa uelewa wamekuwa brainwashed na kuwafanya hizi cheap and stupid terms kama 'mabeberu' zinatumika kuwapumbaza na kuwafanya wazidi kuwa wapumbavu.
 

Viongozi wa kiafrica ndio kikwazo cha maendeleo ya Africa jiulize kwann Africa ilikuwa ikiendelea Kwa kasi sana kabla ya Uhuru na imerudi nyuma baada ya Uhuru vitu simple tu angalia exchange rate,kiwango cha ukosefu wa ajira,uzalishaji,hali ya usalama nk.Viongozi wa kiafrica wanaamini kwenye kutawala watu na sio kwenye kuongoza watu,wanaamini ili kuwatala watu ni lzm uwafanye wawe masikini ( Kusomesha namba) wanaamini ni rahisi kumtawala mwenye njaa maana fikra yake IPO kwenye shibe tu,thus hawataki utawala bora na kuheshimu haki za watu,uendeshaji wa nchi wa pamoja maamuzi yao ndio dira ya nchi zao wananchi hawana nafasi ya kushirikishwa kwenye mustakabali wa kesho yao,wanatumia kodi kama njia ya kuwakomoa watu wanawatoza kodi kubwa ili wengi waendelee kuwa masikini wachache wanaopenya hata wakifika juu ukumbana na vikwazo vya kuwadidimiza sio kuwainua.Wana maneno mengi matamu majukwaani ya kuwaadaa watu Lkn kivitendo hayana uhalisia.
 

Ni zaidi ya wakoloni,heri ya mkoloni mweupe kuliko hawa wakoloni weusi.Africa bila kubadili mfumo au muundo wa jinsi ya kujiongoza toka huu wa sasa ( URAISI) kama ndo mkuu wa nchi tunatwanga maji kwenye kinu heri tuwarudishe wakoloni hata ukiangalia hali halisi achana na somo La historia tulilofundishwa darasani lililojaa chuki Kwa malengo ya walafi wa sasa kutubrain wash toka nje ya box,tofauti ya kimaendeleo kati ya mda waliokaa wakoloni weupe na waliokaa wakoloni weusi ni kipindi kipi kina nafuu.Simple questions mfano nani ni mzalendo halisi aliyeijenga Zimbabwe na nani aliyeibomoa vivo hivo hata Kwa nchi nyingi za kiafrica. Ni miaka 60 sasa tangu Uhuru na miaka 50 kabla ya uhuru .
 
Reactions: Qwy
Ujamaa tulio adopt sisi ulikuwa ujamaa wa kishamba na unaoendeleza hali ya umaskini.

Tukiadopt ujamaa wa kimasikini ukiwa na nadharia ya kwamba uzalendo ni kuwa masikini kumbe ni Kwa malengo ya aliyeuanzisha akiamini kuwatala watu vyema wafanye kuwa masikini nae utatawala vyema
 
Ww hata huelew nn maana ya ujamaa
 
Ujamaa hauwezi kifanya kazi dunia ya leo...na huu ndiyo umewalemaza watanzania wengi (wazazi wetu( hasa walio na miaka 60+ walikulia kwenye mfumo huu huu ...watoto wao sisi tunahangaika hadi kuwakatia bima za afya hawana kitu kisa ujamaa.

Karl Marx aliudanganya ulimwengu.
 
Ww hata huelew nn maana ya ujamaa
Ujamaa ndio huu wa China niujuao, ninyi mnasema China imeshindwa ujamaa mna hitilafu kichwani, Russia ni superpower kwenye military na ni huo ujamaa umewafikisha huko
 

Badala ya kuwaondoa wakoloni tungetengeza mfumo huru wa kuwafaidisha wote
 
Mijira imekatwa
Imekatwa kabisa Kwa wanyonge ikazibukia Kwa wateule wachache hadi wakisaza baada ya kuhonga michepuko na kwenda check up Kwa dola 12M huku wengi tukiimbishwa chorus ya uzalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…