Mkuu Invisible, kwa awamu hii ya utawala tuliokuwa nao,utawala unaonyima haki zote za msingi za kumfanya mtanzania ajisikie huru, JF ndio sehemu pekee kwa Tanzania ya sasa kuwa mtanzania anaweza kutoa dukuduku lake la mayoni hasa kuhusu hizi siasa za vitisho,siasa za ketekana na kupigana risasi..
Nimeona kuna nyuzi nyingi zinazohusu Zanzibar hasa kama zile za Mungano huwa hazichukuwi dakika tano hufutwa wakati kwenye mitandao ya kijamii ya wazanzibari zinajadiliwa kama kawaida,binafsi uwazi na majadiliano naamini ndio njia pekee ya kuondoa tafauti..
Naamini kama tunakuwa wawazi na kuweka vitu mezani na kuanza kuvijadili mapigano,utekaji,kutokuelewana itakuwa hamna,siasa za makongamano,siasa za yakujadiliana ndio zinazofanywa na nchi za Ulaya,Marekani na zile nchi zilizopiga hatua kimaendeleo..
Kama JF mmedhamiria kuwa mabigwa wa uhuru wa kuongea,uhuru wa kujadili,uhuru wa kutoa mawazo na maoni basi wacheni watanzania watoe maoni na mawazo yao kwenye JF kwani hii naamini ndio sehemu pekee mtanzania anajisikia huru,,, kama hamuwezi kufanya hivyo basi bora hii "option" ya "jukwaa la siasa" iondoeni....Nawakilisha