Michoro maarufu

Tokyo40

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,065
Reaction score
1,926
Wafanyabiashara na makampuni wananunua michoro mbalimbali kwa ajili ya investment ya baadae. Kila miaka ikipita, thamani ya michoro inapanda.

Hizi ni baadhi ya picha za wachoraji mbalimbali, mwaka picha ilipochorwa na bei ya mwisho (US Dollars) iliyouzwa katika minada mbalimbali Marekani.

Les femmes d’Alger (Version O)
1955
$179 million
Pablo Picasso




When will you Marry? (Nafea faa ipoipo)
Paul Gaugin
1892
$300 million



The Card Players
Paul Cézanne
$250 million
1890



Three Studies of Lucian Freud
Francis Bacon
$142 million
1969



No. 5
Jackson Pollock
$140 million
1948



Woman III
Willem de Kooning
$137 million
1953



Portrait of Adele Block-Bauer 1
$135 million
Gustav Klimt
1907




The Scream
Edvard Munch
$120 million
1893




Garcon à la Pipe
Pablo Picasso
$104 million
1905




Portrait of Dr Gachet
Vincent van Gogh
$82 million
1890



source:telegraph.co.uk
 
Bal du Moulin de la Galette
Pierre-Auguste Renoir
$78 million
1876




Portrait of Joseph Roulin
Vincent Van Gogh
$58 million
1888

 
Masikitiko makubwa ni kwamba pamoja na michoro hiyo kuuzwa kwa bei kubwa
sana kwenye minada, baadhi ya wachoraji wa picha hizo walikufa kwa umaskini
mkubwa! Huyo Paul Gaugin kwa mfano, baada ya kuona maisha yanamwendea
vibaya ufaransa (ni mfaransa huyu) na uchoraji wake haumlipi vizuri (picha zake
zilichekwa sana) alihamia kwenye kisiwa kimoja huko Tahiti ambako alifia akiwa
maskini wa kutoka ukurutu akijikuna.
 
Hii ndio dunia na walimwengu..ndio maana dhahabu na almas zinakotoka wenyeji ni nafukara na watu wa kati ni matajiri sana
 

Hata Van Gogh pia kafa masikini sana. Aliugua kichaa, kajikata sikio kwa hasira baada ya kugombana na Paul Gauguin (walijuana) na mwisho kujiua mwenyewe kwa bunduki.
 
Portrait of Adele ilichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa Myahudi wa Kijerumani na serikali ya Hitler. Akaibuka Austria. Kuna wakati Austria na Ujerumani waliungana, na hata Hitler alizaliwa Austria.

Familia ya Adele wakakimbilia Marekani. Wakapigania mchoro wao mpaka mahakama kuu na kushinda. Wakairudisha mchoro Marekani na mwisho kumwuuzia Ronald Lauder, kwa dola milioni 135 mwaka 2006.

Ronald mmiliki wa Estée Lauder, kampuni kubwa ya vipodozi duniani na jina la mama yake mzazi.
 
Ila wakuu kibongo bongo upenzi wa michoro kama hiyo bado kabisa. watu hawana upenzi kivile we lete umbeya tu hapa or mapenzi uone watu watakavyotiririka !
 
The famous Monalisa Painting by Da Vinci ipo wapi?
 
Mpaka leo sijawahi kujua maana ya hii michoro. Kwann ibebe thamani kubwa hivyo?
Whats the secret behind?
 
"Masonic influence" sioni hata uzuri WA hizo picha Kama makatuni
 
Naona mapichapicha tu,chenga chenga,mchele mchele,marangi rangi tu.

Huko ulaya naona hela haina kazi kabisaa.
 
"Masonic influence" sioni hata uzuri WA hizo picha Kama makatuni

Kama hufahamu historia ya wachoraji au hujasoma Art shuleni, huwezi kuona thamani ya uchoraji au uzuri wa picha.

Just because you don't appreciate or know little about Art and art history, it doesn't mean it's Masonic.
 
Mpaka leo sijawahi kujua maana ya hii michoro. Kwann ibebe thamani kubwa hivyo?
Whats the secret behind?

Nyumba za makumbusho ni biashara kubwa duniani. Ukitundika michoro ya zamani, unapata wateja wengi kulipa ada ya kuona michoro.

Hii michoro ni investment kama unavyonunua stock ya kampuni. Baada miaka kadhaa, unauza na kula faida yako ukipenda.
Au unatundika jumba la makumbusho na kuwavuta watalii kama wanavyofanya London na Paris na miji mingine.

Jumba la Makumbusho la Louvre la Paris peke yake linapata wageni milioni 9 kwa mwaka na kiingilIo ni Euro 15 kwa wakubwa. Fanya hesabu.

Siyo kila mchoro ni bei kubwa, lakini hamna mtu anapata hasara kununua hapo. Bei huwa zinapanda kila mwaka. Kila miaka inavyokwenda, thamani ya michoro inapanda.
 
yaani mimi mwnyewe sielewi kwanini katuni izo ziuzwe gharama kiasi hicho. mimi naonaga chenga tu
 

Sijakataa kuhusu hizo nyumba za makumbusho.
Ila ukiangalia hiyo michoro hata haivutii useme itakuwa inakupendezeshea nyumba.
Michoro mingine ni kama makorokocho tu.
Hiyo michoro inabeba maana yeyote?
 
Sijakataa kuhusu hizo nyumba za makumbusho.
Ila ukiangalia hiyo michoro hata haivutii useme itakuwa inakupendezeshea nyumba.
Michoro mingine ni kama makorokocho tu.
Hiyo michoro inabeba maana yeyote?

Sidhani kama utaelewa thamani ya michoro kama huna elimu ya michoro au hupendi kuchora.

Ni sawa na mvinyo. Kama huna elimu ya ladha ya mvinyo (Sommelier), hutoweza kujua sababu ya mtu kulipa elfu moja kwa chupa wakati zipo za dola 10.

Ninavyofahamu ni kuwa kila mchoro unabeba maana yake na hatuwezi kujua bila ya kusoma elimu yake kama tunavyosoma somo lolote.

Na nyumba za makumbusho zisingeweza kupata wateja milioni kumi kwa mwaka na kupata dola milioni mia kama wasingeweka michoro hii.

Unahitaji kutumia pesa kuzalisha pesa katika biashara yoyote. Hii ya makumbusho, ni biashara ya dola milioni mia kwa mwaka, hawaoni hasara yoyote kulipa hiyo michoro.

Mwisho wa siku, bei ya kila kitu kinapangwa na sheria za kiuchumi (demand and supply).

Mimi naendesha Toyota Carina lakini mtu mwingine ataendesha Rolls Royce.

Mimi nasafiri Econony Class, wengine wanasafiri First Class.

Kila mtu na uwezo wake na kila kitu kina bei yake katika soko.
 

Hapo sasa tunaanza kuelewana.
Kumbe kuna elimu inatakiwa ili kuielewa hiyo michoro?
Ngoja nianze kujifunza hiyo elimu ya michoro.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…