Habari MMU
Kwenye haya maisha bana wanawake wanajua kupenda sana na usiombe ukakutana na mmoja wao aliyekuelewa.
Wiki jana kabla yakuachana na mchepuko mmoja binti mrembo na mwenye IQ ya wastani nakumbuka alikuwa anaweka malengo na mipango ya mbali sana, kiukweli mwanamke akikukubali anashindwa kabisa kujizuia na yuko tayari kukupa chochote na kutoa ushirikiano ili tuu asikupoteze.
Basi bana dada wa watu alikuwa anashare na mimi mipango yake na story fupi ya utafutaji maana ndio kwanza amemaliza chuo mwaka jana na tayari amepata kazi japo niya mkataba wa muda mfupi, mimi nilikuwa namsikiliza tuu nakumpa support ya kuitikia maana najua kwa kuwa nishakula tunda siwezi fanya nae future yoyote either family au bussiness.
Hii ni kwasababu nilishawahi kufanya biashara na dem mmoja na mwisho alinipiga kama mil 4 hivi na mahusiano yakafa lakini kwa sasa nina familia yangu. Kama kawaida ili maisha yaende mwanaume unaamua kuwa na mpango wa kando for incase lolote likitokea basi unapunguza stress.
Naamini wanaume wengi wenye mke na familia huwa tunapenda kuwa wazi kabisa kuhusu status zetu ili kuepusha jam na usumbufu unaoweza kupelekea mikwaruzano kwenye ndoa zetu.
Kila nikikumbuka zile care najaribu kufikiria kwa vijana ambao hawajaoa au wanaume wenye ndoa zinazokumbana na changamoto za wanawake wao na ukaamua kuchepuka na binti kama huyo je maamuzi yafuatayo ni yapi.....
Kiukweli niliona nimuwekee sababu zakuachana ili apate mtu sahihi watakayepanga maisha angali umri ukiwa mdogo na hilo limefanikiwa na kwasasa niko na amani.
Nakuombea mema upate hitaji la moyo wako.