"michapio bubu"

Mtanzanika

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
2,389
Reaction score
1,131
Nilikutana na uzi unaohusu michapio, katika kupitia nikagundua michapio yote ni ya kimatamshi, nikakumbuka kuna michapio mingine ni ya kivitendo. Labda niiite michapio bubu. Kwa mfano:-

1. Mezani kwako una Desktop na Laptop. Kuna files unataka uzitoe kwenye desktop uzilete kwenye Laptop au kinyume chake. Sasa unajikuta umeshikilia mouse ya desktop unabonyeza bonyeza huku ukitarajia matokeo kwenye screen ya laptop.

2. Umemaliza kuongea na simu sekunde 45 zilizopita lakini bado simu umeishikilia sikioni mwako.

3. Unaendesha gari, ukataka kupunguza sauti ya redio lakini ukajistukia unabonyeza button ya kushusha kioo cha dirisha.

Binafsi ishawahi kunitokea moja wapo, bilashaka wadau na nyinyi mmewahi kukutana nazo..!!hebu tafadhalini jamani tupieni...!!
 
niliwah panda bodaboda nataka kulipa nauli natoa kwenye mifuko ya suruali hela nikaikosa maana nakumbuka nilikuwa na buku5! kumbe niliiweka kwenye mfuko wa shati!
 
Niliingia bafuni kuoga, najimwagia maji kichwani hayafiki ilibaki kidogo nipige makelele kuwa bafuni kuna jini kumbe nilikua nimeingia bafuni na helmet ya pkpk!
 
Niliingia bafuni kuoga, najimwagia maji kichwani hayafiki ilibaki kidogo nipige makelele kuwa bafuni kuna jini kumbe nilikua nimeingia bafuni na helmet ya pkpk!

mamaaaa,wee jamaa unakunywa konyagi pori
 
Nilitaka kumwazimisha jamaa kalamu lakini bila kutazama wala kumtazama nikazamisha mkono mfukoni ile kutoa kumbe sigara Sportsman!!
 
nimezoea kuendesha gari iko siku nilichukua vespa nikataka kuangalia nyuma nikaangalia mawingu mana nilidhani kuna kioo cha ndani
 
Nilikua nataka kunya ukatoka mkojo peke yake
 
Tuliambiwa tushuke kuchimba dawa nikaanza kununua nyama pale mbele ya panda ya mzumbe hadi muda ukaisha
 
Nilikuwa natafuta miwani baadaye nikaamua kumuuliza ps wangu miwani yangu iko wapi? Akanijibu mbona umeivaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…