Una mistari ya kitoto kama ae iou,Ona uyu fala,ulimi kama ndala//
Flow za kishamba,zinanuka kama jalala//
Vipi haujala,Au jana hukulala//
Kusmoke sio ujanja,kichwa kama embe//
Hata mimi nakula unga,ila ni dona na sembe//
Mistari haieleweki,au dogo unakithembe//
Mwembamba kama wembe,Kenge nakuachia kimbembe//
Sauti yako laini, kaza kama Edo kumwembe
Kidume unaitwa kwini,Tutakuvisha bikini//
Tukule mpaka maini,Kuwa makini....
Mcqueenen
Una mistari ya kitoto kama ae iou,
Ataeona una uwezo lazma awe kipofu,
Tena kipofu kilaza, mathe awe below 2
Mi nachana ngumu afu we bishoo 2
Mi naitwa rungu, nikipulizwa ni kifo Cha mende
We unaitwa mk**du, mwli mzima hauna makende
Mimi sio Mungu, hiyo nmejuaje? Kwasababu unaitwa kenge
Na sifa ya kenge ni mtundu, ila hajui mahindi ndo sembe
Hajui wahindi sio wazembe
Hajui TP ndio Mazembe
Hajui ukimuita Manala sope haji
Halafu kenge sifa kuu ni mjuaji
Akiona mvua anajikinga ndan ya maji
We kipofu ila eti unajiita mtafutaji.
Huwezi nizidi bars kichwa hujakichaji
ila usije ukakiplagi maana we ni ritadi
Huchelewi kufanya jambo bila kulijaji
Una tabia za kike umekosa tu sketi
Af unajikojolea kitandan kwako siketi
Kichwa chako kinazidiwa akili na tikiti
Uliloshindwa kupanda kisa huna tiketi
Niishie hapa nikiendelea najiaibishaFlow
hazisomeki,Vina havieleweki//
Unajiita mgumu,wakati mlaini kama Keki//
Punguza hasira,jazba ona sasa umeshapanic//
Hujui freestyle,labda uvae kanga za kaniki//
Vyangu Vina vinaelewaka,kama pilau la iriki//
Wadau wanakuchora,kina eriki na sadiki//
Wanakuona mkora,Domo kama Azizi Ki//
Majirani wamekuchoka,pigo zako hazieleweki//
Mods wanakuchora,acha matusi na kiki//
Member wanauliza,"Au we sio riziki"//
Bado haifahamiki,Ni kama mlio wa pikipiki//
Mtoto unae jigamba, ngoja nikukate wenge/Flow za kishamba,Bora urudi shamba//
Uwezi kutamba,huu ndo ukweli,Sikupigi kamba//
Usipoelewa utajilamba na ukikaa vibaya Utalambwa//
Usijitie ujuaji,Ukawa kama Haji,tukamfukuza Simba//
Unaulizia bei ya ford,wakati hata bando uwezi afford//
Dogo piga kitabu komaa,usiwaze kina Shamsa Ford//
Ukileta mzaa,tutakutoa Day tukupeleke board//
Ukifaulu vizuri,Babaako nakupeleka Abroad//
Sasa ongeza Juhudi,Kwa uvumba au udi..//
Nasema uongo wanabodi??
Umetisha mkuu😆😆Life ni kubattle/na usiogope kuishi gheto/ogopa watoto warito/ufunge ndoa na punyeto/usijeishia kula msoto/usijifanye we mnato/na usiogope changamoto/ujana maji ya moto/piga kazi isiwe majuto.
nchini tumevamiwa afuu kuliko sharrif MajiniKwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forums, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
Hilo goma nalikubali sana.Leo naona bora mvua
Kesho naona bora jua
Uko wapi dr mwenzio ugonjwa utaniua
Kwenye joto siwezi Kaa
Baridi ndio balaa
Khaaa
Siwezi kula
Ingawa nahisi njaa
Sina hela ka wenzangu ila kusaka naweza
Nachpatanamshukuru bora siku naisogeza
Unanipa wakati mgumu akili naenda
Slow sloo
Haunipi ushauri km ilivyokuwa before befooo
#Chiku K
Malizia kuichanaHilo goma nalikubali sana.
Da umenikumbusha Mbali sana , Kipind naimba mziki/Kwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forums, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
Hii iko poa MkuuDa umenikumbusha Mbali sana , Kipind naimba mziki/
N'likuwa best kwa kuchana,Na mitaa ikanibariki/
Niliandika kwa mapana,Sio notepad ilikuwa biki/
Japo sikujulkana,Ila nilizoa mashabiki/
So sasa ni uhumi mtupu, Na tumejigeuza kondoo,/
Waguse wakupe upupu, Hawashauriki ka jogoo,/
Na wengi ustaa wa loop, Hiphop hawaiwezi noo,/
We Mvumbo karibu supu,maana umenikosha rohoo(roo)/
Nilikuwa pozi tu kitambo,Kabla sijakimbia majuu,/
Enzi hizo mkali bambo,na anachana Mr two (tuu)/
Shida za mama wa kambo,kabla haijafutwa tambuu,/
Taarabu mziki wa Tambo, Kidogo nasma n' mama zuu,/
Sasa hivi tambo mipasho,Kwa rap kama ushenzini,/
Wachache wanaitolea jasho,Ila amapiano iko enzini,/
Wengi wanaingia huku magasho,Ndo wanachoharibu scene,/
Hiphop inahitaji fusho, thanks Khali mwenye graph mjini,/
Mwenzio napata tabu, Usiku kwangu ghadhabu,lonely/Malizia kuichana
Kule anachana Chidi
Bado kwenye mic Niko mbele kama titi...Chid kwenye one and 2 spitts some realy Sh#$**t
View attachment 2746717