Michano/Hiphop/Freestyle

niameani Mademu wa siku hizi bila pesa huwapati/
leo kuna demu kumwomba game anadai mpaka nimtoe lunch
si nikwamwbia okay baby basi twende kwanza tukale breakfast/
kakubali kishingo upande japo kanipa masharti/
anadai anataka akifika akute supu ya kuku pamoja na chapati/
na me mfukoni nina buku mbili miatano na bati
kumchana ananitukana na kuniita eti me ni fataki/
Ama kweli mademu wakali bila pesa huwanasi
 
niite comrade ndio langu jina,me ndio mkali wa kuflow wananiita master wa vina/
nimekuwa famous broh hip pop imelikuza jina,ma snitch zina wauma roho natambulika jiji zima/tena sishindani na hao makima/maana nikiwapea mistari 3 tu wanazima/now nina power kama john cena/wakisikia jina langu mikia inafyata wanakaa kimya
 
nigga usipambane na mimi kama huna bima,comrade ndo master wa vina, flow zimeninata nikitembea namwaga mistari jiji zima/
na nimeshaveshwa crown, so siwezi battle na watoto leteni watu wazima/
na flow kama doni mistari kama nimetokea mamtoni,nikipandwa mzuka naweza flow hadi kichina/
 
niameani Mademu wa siku hizi bila pesa huwapati/
leo kuna demu kumwomba game anadai mpaka nimtoe lunch
si nikwamwbia okay baby basi twende kwanza tukale breakfast/
kakubali kishingo upande japo kanipa masharti/
anadai anataka akifika akute supu ya kuku pamoja na chapati/
na me mfukoni nina buku mbili miatano na bati
kumchana ananitukana na kuniita eti me ni fataki/
Ama kweli mademu wakali bila pesa huwanasi
Siku hizi mapenzi ni pesa, jipinde mwanangu Comrade/
Vinginevyo utaishia kupepesa, pisi kali utawaita shemeji/
Ukichanganya madesa, utaumia na hutafungwa bendeji/
Watakuona kama rumbesa, wanapiga spana kama gereji/
Watoto wanataka noti/ ndiyo ushtue kijoti/ wakajaze hot pot/ pizza na marosti/ bure inawakosti/ ya wigi kwa shost/ rabda upate kina Kidoti/ upewe ugali wa kupiga goti/
Pesa sio Dini, ila inatupa kiwewe/
Kumbuka mke wa masikini, kuwadi ni mumuwe/
 
Mvumbo mademu wa siku hiz niku hit then una run,ukifwata mkumbo watakuchuna pesa hadi utalani/
shida yao nikushibisha matumbo na mapenzi kwao kama utani/ ukiwa na pesa watakuonyesha upendo usio na kifani/
ila hawana true love wengi wao ni makahaba, bila ela hupewi kitu zaidi ya mabusu tu labda/
 
CANABINO
iamconboi___B-1ZcOSDj3O___.jpeg
 
bongo ukijifanya mwana harakati kama roma, utapigwa amberkati uliwe kisodoma/
Na wabongo wengi ni wanafiki kinoma, wanajifanya wanakupenda kumbe wanakufanyia mikakati kwa sangoma.
Yaani kuishi Bongo homa, maskini jua linatuchoma viongozi wanakula mgao wa corona/
 
Me ndo great rapper, sishindani na hao rapa vichwa kapa/
Na natunza culture, kama rapture me ni rasta sili nyama ila nakula bata/
Nipo fasta sio siri snichi wamedata, na nikifa nita acha pengo kama mkapa.
 
Uzi umefika tamati, na mbishi nimekuja../ nawa donoa kwa vyenga hatari, niite scars lapulga.../

Nawakilisha tz bara, hadi visiwani unguja.../

vina vyangu ni imara, na sio fake kama nguo zakuchuja.../
 
wahuni kila kitu tuli fanya, mitaa ilitufunza chocho zote hadi njia za panya/
maisha siku hizi yame bana, uhuni sio sifa tena tafuteni kazi za maana/

usipo ajiriwa usitukane serikali, kaa chini tumia akili kutafakari/
maisha ni kama safari, na upo ndani ya mtumbwi unakatiza kwenye bahari/
unataka kufika mbali, changamoto ni nyingi inabidi ujihadhari/
 
wahuni kila kitu tuli fanya, mitaa ilitufunza chocho zote hadi njia za panya/
maisha siku hizi yame bana, uhuni sio sifa tena tafuteni kazi za maana/

usipo ajiriwa usitukane serikali, kaa chini tumia akili kutafakari/
maisha ni kama safari, na upo ndani ya mtumbwi unakatiza kwenye bahari/
unataka kufika mbali, changamoto ni nyingi inabidi ujihadhari/
Mitaa imetulea now tumekua, japo elimu ya mtaani tunayo lakini bado hatujatusua

Endelea ku fight wanangu piga sana dua, life ka kombolela iliushinde we butua.../

Fikiria njia za kupata pesa ila sio kuua, mwisho wake ni mbaya wengi wameangukia pua.../
 
Huu ni muda wa kumbonji, naweka simu kando nizivagae njozi.../

Bible pembeni siguswi na walozi, joto kali geto sina kiyoyozi.../

Mbu wako na mimi, net imetoboka, konani kuna mpini, mwizi itakukosti uki shoboka.../
 
Hawa rapper sasa ni wepesi kama flu, kichwani wapo kapa wanabebwa na beats tu/
mtaani wanajitapa wakipewa mike nothing they can do/
sasa nawapiga msasa coz hawauwezi mziku huu, nimeshawasha stata nawapindua chini juu/
 
Usiku mwema kwenu mabibi na mabwana, mlio na bahati na wenye laana.../

Nawaalika katika maombi ya geto, yawafikie mlale salama muepushwe na mapepo.../

Kama ni maskini usiwe na gubu, napiga gosple ili asubuhi uvunje kibubu..../

Pitisheni sadaka hii ni ibada njema, maana nawaombea hadi mawack wapate neema.../

Kama nawaboa mnasema, nikatisha maombi niwaache na sinema.../
 
Nacheza kama Pele, kila dude nnalotupa ni ushindi/
Nasmama mstari wa mbele, hata wakinicheki kama Philipo Nyandindi/
Nipo kwenye kilele, toka wako shule ya msingi/
Hawaniwezi hawa mchele mchele, rabda waniendee Giningi/
Nimewateka Kiarabu/ wanatetemeka kama Waziri wa Magu/
Siku zote kuku hawindwi, japo huponzwa na rangi yake/
Na kumbuka Tembo hashindwi, nguvu na mkonga wake/
 
Mchumba kanitenda sina mkwanja, kadata na nyangema mkesha viwanja.../

Sikufichi binti nilimpenda sana blaza, upendo ulikufa nilipomfuma na mwana china plaza.../

Kama ni msosi home wakusaza, kitandani nilihakikisha namfikisha kila tulipoanza.../

Now kani cheat, mwili umekosa nguvu kiufupi siko fit.../

Natafakari njia ya kisasi, nahisi labda itapoza nafsi, maana adhabu kwa muhasi ni kufyatuliwa risasi.../

Ila naona bado haitanipunguzia hili jeraha, maana nitayakabili maisha ya pili ya jela.../
 
njiani akitembea anakata makalio, nikampotezea nikajikita kusaka salio.../

kwa ule mkuki nilochomwa na yule mfilisti, nilijenga chuki wanawake wote nikawaona wasaliti.../

Kwenye kiti cha moyo wangu mwanamke hakua na siti, ila siku zilivyosonga nilijikuta nimekua peace.../

Maumizi yakuachwa yalikoma, nikafungua ukarasa mpya wa mapenzi nakuanza kusoma.../

Iliikua ni furaha iliyopotea muda umbali mrefu, kumpata mwanamke mwenye akili pevu.../
 
Nyie watoto kwa rap bado sana, bars mbili mnajiona mpo gado sana.../

Dj afro mtego Wa scars umemnasa rambo chacha, unapoteza muda kunishtaki kwa mambo sasa.../

Hii ni vita sio battle blaza, kwenye spika naskika mpaka chattle mwanza.../
 
Back
Top Bottom