Habari za jumapili wana MMU,
Napenda kuuliza jambo moja kuhusiana na hii dhana ya hizi marriage anniversaries.
Lets say ulifunga ndoa miaka 50 iliyopita, lakini baada ya kufunga ndoa, mlikaa miaka 10 mkaachana, kila mtu akaendelea na maisha yake (possibly mume ukawa na mke mwingine au mke akawa na mume mwingine), baada ya miaka 15, ikatokea mkaamua kurudiana, mkaanza kuishi tena kama mume na mke, swali ni je, mtajitanabaisha kwamba mna miaka 25 ya ndoa while 15 mliitumia mkiwa mmetengana? Na mkiendelea kuishi hadi ikatimia miaka 50 tangu mmefunga ndoa, je mna uhalali wa kusema ndoa yenu ina miaka 50?? Nawasilisha!