Miaka 31 sasa bado ninakuona ndotoni

Luck-12

Member
Joined
Jan 16, 2022
Posts
62
Reaction score
75
Ulikuwa rafiki mzuri kwangu, sauti nzuri na mwenendo wa kufaa kuwa mke mbeleni, masomo yaka tuweka mbali Malkia, hatukuwa na simu, kama walizonazo hawa, na pia hatukuwahi (kujuana) kama wanavyo juana vijana wa sasa.

Ila nashangaa tangia tumalize shule bado naiona sura yako Malkia, ingawa nina maisha mengine na mtu mwingine, sijui ulipo, upo hai, au ume tangulia.

Jua, tambua Malkia unakumbukwa, salaamu zikufikie.

Ndimi Hp
 
Sasa hv amezalishwa na ameachwa single mother wa watoto wanne.
 
Kwa hiyo uzi wake ni kwa hisani ya genye?
Ah, hiyo iko wazi kabisa.
Sasa mtu more than 30 yrs badala ya kuhangaika na mawazo ya kulipia watoto ada n.k ye anahangaika na "malkia" hapo no obvious yuko anavuta tu hisia ajikung'ute cha kulalia.
 
Kwa haraka haraka utakua hukosi miaka 45 hivi labda, moja kwa moja ulikosea kuoa mkuu ama Huna furaha na ndoa yako ndio jambo naweza kukuambia[emoji28]

Maana kama ungeoa mtu sahihi wala hizo kumbukumbu za miaka yote hizo zisingekutesa mpaka na Leo aisee!!

Wekeza mawazo kwa mke wako mkuu, la sivyo ukikutana na huyo malkia na akiwa ni mama wa hovyo kuna uwezekano ukakuvunjua ndoa yako kirahisi kabisa!
 
Ukiona unamuota ex wako kila mara Ina maanisha haupo happy na mpenzi / mke / me wako wa sasa yaani ahaa bora liende tu kwa sababu ya watoto.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…