Mheshimiwa Msigwa ndani ya Dk 45 ITV

Mmbea tu kwa nini asiwataje kama anawajua anatafuta sifa za kitoto.

Usiwe kama shoga acha kubisha hodi chooni, anayetakiwa kuwataja ni waziri wako wa mali asili. Kama waziri wako kashindwa kuwataja unategemea nini?. Istoshe kesi ziko mahakamani kwa hiyo kutaja mtu ni kuingilia kesi iliyoko mahakamani. Kwa kitaalamu wanasema "Without projudice" kama itabidi kufanya hivyo na nilazima atangulize neno hilo.
 
Mmbea tu kwa nini asiwataje kama anawajua anatafuta sifa za kitoto.

Lumumba kaaazi kweli kweli! Hivi mnataka mtajiwe nani wakati alisha mtaja King Maker Kinana pale Bungeni. Tulicho kishuhudia ni wabunge na mawaziri wote wa MAGAMBA kutokwa povu badala ya kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kupata sehemu ya kuanzia uchunguzi!!!

Meno yamepitishwa bandarini na kampuni yake. Yakasafirishwa na kampuni yake. Meno yaka kamatwa, cha ajabu mwenye mali akawa hajulikani.

MKAMATWA NA NGOZI SI NDIE MUIBA NG'OMBE, eti?
 

Kwani hajawahi kuwataja? Kuna msomali Kinana na Lukuvi. Au nawewe huwajui hawa?
 
Mmbea tu kwa nini asiwataje kama anawajua anatafuta sifa za kitoto.

Tatizo mnakesha lumumba ndio mana hamna kumbukumbu. Nimara ngapi amewataja akiwa bungeni na kwenye mikutano? Nakushauri uwe unalala waweza kua na akili.
 
Kwani hajawahi kuwataja? Kuna msomali Kinana na Lukuvi. Au nawewe huwajui hawa?

Kama aliwataja kwanini asiwataje Tena na tena mpaka tukamuelewa !Mi nashangaa sana ,kabakia wanajulikana wapo keko ,ubungo ,kibandamaiti ,,hakuna jina ,sasa anaogopa kitu gani ,kwani wale mafisadi si walitajwa mchana kweupe kwenye mkutano na hao hao CDM ,labda kama alivyosema mfuasi mmoja humu kuwa kesi zipo mahakamani ,hapo panakamatika.

Nimeona udhaifu wake pale aliposema au alipoulizwa , Je kama ni wewe ,kama ni wewe ndio Waziri husika ungechukua hatua gani ? Yaani hapo ndipo nilipomuona jamaa hajui atendalo au analolihubiri ,anaenda kusema eti nitamuendea bosi wangu na kumwambia nahitaji kufanya ,1,2,3,4 na tano , amewateta waziri ,halafu yeye anasema atamuendea raisi !!!

Ndugu umeshapewa dhamana ya Uwaziri kutekeleza majukumu yako inabidi umuendee Raisi,unamuendea Raisi kufanya nini au akufanyie nini ! unaenda kutafuta ushauri ! unaenda kuomba ruhusa ! unaenda kufanya nini ? ,sasa huo Uwaziri utakuwa na faida gani kwako na WaTanzania ,hapa nimemuona kavuruga kila kitu ,,kwa nini asiseme nitawachukulia hatua kali wale wote watakaobainika na kuhakikisha wanafikishwa mbele ya haki ,jambo ambalo alilitetea mwanzo kwa kuvilaumu baadhi ya vyombo kama TANAPA na vingine.

Sasa mtu wa aina hii anaesema nitaenda kusema kwa Raisi kaono hili na lile na anaona afanye hili na lile ,huyu jamaa si atamtosa raisi wake na yeye kujiweka mbali ,yaani hawa ndio wanaotarajiwa kushika uongozi ? kweli bado Chama kichanga..
 
Katika wabunge...MSIGWA nimemkubali. Nimeangalia kipindi chote jamaa anaongea points...bravo
 

Kuna haja gani yakurudia kuwataja? Je alipowataja nihatua gani serikali iliweza kuwachukulia hatua? Serikali ya chama cha majangili.(ccm) imeshindwa kuwachukulia hatua kwani wao ndio wahusika wakuu wa ujangili huo.
 
Kuna haja gani yakurudia kuwataja? Je alipowataja nihatua gani serikali iliweza kuwachukulia hatua? Serikali ya chama cha majangili.(ccm) imeshindwa kuwachukulia hatua kwani wao ndio wahusika wakuu wa ujangili huo.

Unapolaumu usilaumu mara moja au mbili ,unalaumu zaidi ya mara mia ,hivyo kuwataja na haswa ilivyokuwa kupitiaa ITV ,kwani una uhakika kuwa wengi wa watu wanasikiliza na kutazama ,na kuna msemo mupaka kieleweke ,sasa kuwataja kila wakati sio kosa ni lazima watajwe ,, wenye kosa ni wale wasiochukua hatua baada ya wahusika kutajwa

Yeye asione kosa kuwataja hadharani kila anaponafasika ,ikiwa tu anauhakika nao na ushahidi anao basi awataje,lakini kutaja mara moja tena kwenye vikao vya bungeni hio haitoshi kwani pale bungeni ni sehemu iliyojaa visa na mikasa pamoja na vichekesho sasa huoni kama kuwataja hapo bungeni ilikuwa ni kuchekesha wanaosinzia ?
 

Mkuu hapo itakuwa noma sana mafisadi wakitajwa tu hapo ITV kutazuka balaa umesahau ya Mengi na Manji?
 

Wewe kwa upande Wako unadhani Majangili wanajulikana au hawajulikani?
 
sizani kama unaelewa walicho mwitia hapo kwenye kipindi hawajamwita ataje majangiri mwenye dhamana yakuwataja ni wazili kama hujui yeye kaziyake nikufafanua na kumwambia wazili afatilie

Mwiba anataka Msigwa afanye kazi ya Waziri. Ukiwa mwana CCM unakuwa na akili za maiti

CC😡kamandamakini.
 
Last edited by a moderator:
Mmbea tu kwa nini asiwataje kama anawajua anatafuta sifa za kitoto.

Una kichwa kigumu wewe, kakwambia alishamtajia waziri na serikali yake lakini WANABEZWA na hawawachukulii hatua wala polisi haikuwahi kumshtukia ili atoe ushahidi. unayafahamu hayooooo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…