MHASIBU wa Klabu ya Simba, Erick Sekete Jumamosi wiki hii ameavamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa zaidi ya Sh7 milioni. Fedha hizo zilikuwa ni za mgao wa klabu hiyo ilizopata katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Sinza. "Ni kweli, tukio hilo limetokea mhasibu wetu, Erick alivamiwa na watu waosiojulikana wakati akitoka Uwanja wa Taifa kwenye mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Tusker Kenya. "Ameporwa kiasi cha Sh7 milioni, mgao wa mechi ya kirafiki dhidi ya Tusker," alisema Kamwaga. "Wakati Erick akikumbwa na tukio hilo alikuwa pamoja na Stanley Philipo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yupo hapa Simba kwa ajili ya masomo kwa vitendo ya mawasiliono ya umma," alisema. Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kituo cha Polisi Magomeni ambapo sasa suala hilo linashughulikiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Polisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na watalitolea ufafanuzi baadaye. "Tumepokea taarifa ya tukio hilo, tutalitolea ufafanuzi baadaye," alisema Kinyela.
source gazeti la mwananchi
Maswali ya kujiuliza ... amepokea pesa akiwa uwanja wa taifa... ananyang'anywa sinza Makaburini ... hivi huko TFF wanautaratibu gani wa kulipa malipo kwa wadau wao? huu utaratibu wa kutumia hundi ni wa kizamani au ndo wa kisasa.. vipi namna nyingine za ki - mtandao za kulipana pesa hazipo?
sinza ulienda kufanya nini ?Ni yeye kazichukua; Yaani Unakwenda KUPOKEA CASH MONEY? nilidhani WANAPEWA CHECK na FAT?
KWELI TUMERUDI NYUMA....
Ni yeye kazichukua; Yaani Unakwenda KUPOKEA CASH MONEY? nilidhani WANAPEWA CHECK na FAT?
KWELI TUMERUDI NYUMA....
MHASIBU wa Klabu ya Simba, Erick Sekete Jumamosi wiki hii ameavamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa zaidi ya Sh7 milioni. Fedha hizo zilikuwa ni za mgao wa klabu hiyo ilizopata katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Sinza. "Ni kweli, tukio hilo limetokea mhasibu wetu, Erick alivamiwa na watu waosiojulikana wakati akitoka Uwanja wa Taifa kwenye mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Tusker Kenya. "Ameporwa kiasi cha Sh7 milioni, mgao wa mechi ya kirafiki dhidi ya Tusker," alisema Kamwaga. "Wakati Erick akikumbwa na tukio hilo alikuwa pamoja na Stanley Philipo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yupo hapa Simba kwa ajili ya masomo kwa vitendo ya mawasiliono ya umma," alisema. Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kituo cha Polisi Magomeni ambapo sasa suala hilo linashughulikiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Polisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na watalitolea ufafanuzi baadaye. "Tumepokea taarifa ya tukio hilo, tutalitolea ufafanuzi baadaye," alisema Kinyela.
source gazeti la mwananchi
Maswali ya kujiuliza ... amepokea pesa akiwa uwanja wa taifa... ananyang'anywa sinza Makaburini ... hivi huko TFF wanautaratibu gani wa kulipa malipo kwa wadau wao? huu utaratibu wa kutumia hundi ni wa kizamani au ndo wa kisasa.. vipi namna nyingine za ki - mtandao za kulipana pesa hazipo?
..... Maajabu ... sana ila mkuu hapo kwenye RED siku hizi wanajiita TFF.... FAT zamani... anyway ndo walewale......
.....Halafu nchi hii ni ya ajabu sana mambo kama haya wahusika wanayafuuzia na utashangaa itakuwa ndio mtindo... leo kaporwa wa Simba ..kesho wa Yangajamani sidhani kama kuna kiwango maalumu cha kuomba ulinzi wa polisi hata kama mhasibu huyo ana fikiria kianolgia zaidi jamani in maana hata matangazo ya kufikiri kidijitari haja sikia poleni sana