MH.PROF NDALICHAKO

JOSE KASANO

Senior Member
Joined
Apr 23, 2013
Posts
122
Reaction score
95
Prof Ndalichako mi nitamkubali kuwa ana nia kweli ya kuboresha ELIMU ya nchi iwapo atafanya yafuatayo kwa uchache wake:

1. MITIHANI YA KUHITIMU DARASA LA
SABA.
Prof abadili mfumo wa mitihani ya kuhitimu darasa LA SABA KUTOKA kuwa na maswali ya kuchagua tu ili uwe kama wa zamani au kuboresha zaidi.Hiu itasaidia kupata wanafunzi clean kwenda sekondari.Watoto wengi wanachaguliwa sekondari ni matokeo ya mitihani ya kusiliba ya darasa LA saba yaani wanachagua hadi hisabati.Kila kitu ni
A,B,C,D,E. Hata asiyejua kusoma anaweza kuangalizia herufi na kusilba.Matokeo YAKE sekondari anakwenda kushangaa tu.Hisabati anaambiwa solve,Kiingereza ndo sshida tuupu.
Mfumo huu tafadhali prof ubadilisheni.Zama za waende WOTE mzifute.

2.SIFA ZA KUJIUNGA SEKONDARI.
Selection za wanaojiunga na sekondari iwe ni kwa waliofaulu tu wasiofaulu waachwe au wapewe muda wa kurudia darasa LA saba.Sasa hivi wanasomba karibia wote hadi wengine kusoma ni shida.Sekondari wanaanza kufundisha kusoma na kuandika.

3. VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA.
SHULE zipewe vitabu vyenye mashiko kuliko hivi vilivyogawiwa juzi na kufedhehesha nchi yetu.Eti the big city of Tanzania is Dodoma.Halafu kitabu cha taasisi ya ELIMU.Vitabu vingi vina makosa hata vya sekondari huwezi kuvitumia darasani kama siyo WALIMU kujiongeza au kutumia vya waandishi binafsi.

3.KUPAMBANA NA MIUNDO MBINU YA SHULE.
Wizara ihakikishe SHULE zote za umma zina miundo mbinu yote inayotakiwa.Zipo sekondari ambazo hazina UMEME,MAKTABA,MAABARA,OFISI ZA WALIMU, VITI NA MEZA NK. SHULE hizi zina hali mbaya mno mama yuko kimya tu.

4. KUSIMAMIA MASLAHI YA WALIMU.
Huwezi kuzungumzia ELIMU bora kabla hujashughulikia maslahi ya WALIMU.WALIMU wanadai mishahara, increment zao hawajapewa mwaka wa tatu tunaenda,madaraja kwa sasa ni hadithi kwao, mishahara ni ileile ya zamani ambayo haina uhalisia na maisha ya sasa.Prof Anapaswa kulishughulikia pamoja na wizara za TAMISEMI,UTUMISHI NA WIZARA YA FEDHA.WALIMU wako mazingira magumu sana ya kufanyia kazi,WATIENI MOYO BADALA YA KUWAKATISHA TAMAA.MSISEME HAMTAWAONGEZEA MISHAHARA BADALA YAKE WAPENI MATUMAINI.

5. KUACHA VITISHO DHARAU KWA WALIMU.
Prof Ndalichako muda mwingi amekuwa akiutumia kuwatisha WALIMU na kuwadharau eti hawana content na juzi amesema WALIMU wana vyeti vizuri lakini kichwani Hawana kitu.
Hizi ni dharau kubwa mno kwa WALIMU na wala haziwajengi kisaikolojia kupambana na mazingira mabovu ya kazi.Sijui kama anafahamu mazingira ya WALIMU ya kazi hapa nchini.
HAPO MAKONDA NDO HUWA ANAWAZIDI CREDIT WOTE KWA KUWA PROBLEM SOLVER.
NI KWELI MAKONDA AKILI YAKE HATA KAMA INGETHIBITIKA HANA CHETI UBUNIFU WAKE UNA FAIDA KUBWA KWA NCHI KULIKO HAWA WASOMI WALIOJAA VIBURI NA DHARAU.

WALIMU wajengewe saikolojia chanya ya kufundisha kwa moyo lakini kila kukicha wanakatishwa tamaa tuuuuu.Eti anataka kufanya uhakiki wa akili yao.Huyu prof anaweza kuwa anguko LA ELIMU hapa nchini au anataka kuungana na Bwana wa Buguruni? Maana tulipofikia MTU akisema ni Prof itabidi tuwaogope bora wasiojua kusoma sasa.

6. WALIMU WAENDELEZWE KITAALUMA.
Badala ya kusema WALIMU hawana maarifa ni wajibu wake kuwaendeleza KITAALUMA.
Wapo WALIMU ambao kwa gharama zao wamekuwa wakijiendeleza hadi ngazi ya MASTERS tena za ELIMU lakini eti serikali hawaitambui.Madhara YAKE wasomi hawa wamekuwa wakiendana kwenye fursa zingine tofauti badala ya kuwatumia kwenye ELIMU kutoa mchango wao.Wale wanaotaka kwenda vyuo vikuu ndo wamebanwa hawawezi tena.Kwanza ruhusa ni shida wanaambiwa labda waache kazi.
Prof apambane WALIMU wenye masters watambuliwe na kuthaminiwa.

7. KUTOFUNGA VYUO VIKUU.
Huwezi kuboresha ELIMU kwa kufunga na kufuta vyuo vikuu. Hii siyo sawa,vyuo mvifungulie vifanye udahili ila wekeni mfumo wa kudhibiti ubora wa vyuo vyote. Kufungia vyuo kumesababisha vijana wengi wenye sifa kukosa vyuo.Bado tunahitaji wasomi.Kumbukeni nyie mkitoka ni kina nani wataendesha wizara kama siyo hawa mnaowadhibiti kupata ELIMU ya juu.
HAYA YAKIWEKWA SAWA ANGALAU TUNAPATA PA KUANZIA KUBORESHA ELIMU YETU.

NI MTAZAMO NIONAVYO MIE KWA MAKENGEZA.
 
Kinachofanya elimu yetu iwe mbovu ni kitu kimoja tu [UMASKINI]
Hata aje malaika mtakatifu kwa bajeti zetu za kimaskini huwezi kupata elimu bora,
Ili walimu walipwe vizuri inahitajika fungu la kutosha
Ili miundombinu ya shule, vyuo na taasisi iendane na ubora zinahitajika pesa nyingi.
Kuandaa walimu bora watakaofundisha shule bora wanahitajika wahadhiri bora na vyuo bora, yote haya yanahitaji massive investment.
 
"Sikuchaguliwa Kuongeza Mishahara ya WafanyaKazi Nimechaguliwa Kuwatumikia Wananchi Wanyonge Wa Tanzania "
 
You are the great thinker [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji106] [emoji106] maana hali ngum sana kama mfumo wa elimu utaendelea hvyo std 7 kuendelea kushade Abcd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…