Mgombea wa Kiti cha Urais pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Haji Ambari Khamisi, wachukua fomu ya uteuzi katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi leo Agosti 15,2025.
Mwishoni mwa mwezi Machi, NCCR-Mageuzi kilimteua Haji Ambari Khamisi kuwa mgombea wake wa urais, akishirikiana na Joseph Selasini kama mgombea mwenza.
Khamisi, mwanasiasa mkongwe, aliahidi kurejesha heshima ya Chama hicho kama ilivyokuwa 1995 chini ya Agustino Mrema.