Mfumo wa Utawala

mchonga

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,233
Reaction score
249
Nimepata hii toka kwa mdau wa UK ningependa Tu-share



Ukisoma yote niliyoyoandika utaielewa nia yangu njema…..

Leo naandika si kwa sababu ya mapenzi ya kuandika, bali kwa machungu yatokanayo na kutoandika nidhaniacho kinapaswa kueleweka wazi kwa kila mwanadamu anayeishi au kutoka ktk vinchi vyetu hivi masikini.

Naandika nikiwa na imani kwamba kila anayesoma ujumbe huu, ameishawahi kulalamikia mfumo wa utawala wa nchi yake kwa sababu za wizi, ubadhilifu, ufisadi, uonevu, ukandamizaji, uzembe, upendeleo, ujinga, huduma (za elimu, afya, mawasiliano n.k) duni na orodha inaendelea.

Naandika kwa sababu nina nia madhubuti ya kukusuta wewe unayedai kuudhika na mifumo mibaya ya utawala na uongozi ktk nchi husika pasipo kufanya lolote kuleta mabadiliko na maendeleo ktk jamii yako na badala yake unabaki kulalama tu.

Mpendwa msomaji napenda nikuelezee kwa mtazamo wangu binafsi, ni nini cha kufanya ili kufikia maisha bora ktk jamii zetu. Nitafanya hivyo kwa kutoa mifano dhahiri kutoka ktk ulimwengu wangu wa sayansi na technologia. Nitaoanisha mifano hiyo na mifano ya mambo mbalimbali ktk maisha ya kawaida tunayoishi na nitakuachia wewe uamuzi wa ni lipi bora, …yaani kukaa kimya au kushiriki ktk sakata la kuleta mabadiliko yako na jamii yako.

…Hakika ni wazi uandaapo uji au chai ya kunywa, pamoja na kupasha moto ni lazima ukologe kupata mchanganyiko bora. Kama si kukologa basi ni wazi mchemko unatosha kufanya kazi ya kuchanganya. Hii ni kweli pia kwa michanganyika mingi ya kisayansi na isiyo ya kisayansi. Ukologaji huu una kipimo chake kwa lugha ya kisayansi yaani “Entropy” au kwa kiswahili ni “kipimo cha vurugu” ktk hatua za uchanganyaji. Ukizidisha au kupunguza ukologaji hautapata mchanganyiko mzuri unaotakika.
Vurugu hizi, yaani “Entropy” zinathibitika pia katika utengenezaji wa vitu kama vile smooth juice, togwa, bia na orodha inaendelea.

Zaidi, vurugu hizi zinathibitika kwa watu wanaotumia kiasi cha moto kufukuza (si kuua) nyuki ili wapate asali. Ukiwapigia kelele nyuki kwa lengo la kuwafukuza upate asali, nadhani jibu unalo wewe mwenyewe.

Vivyo hivyo katika safari kuelekea maendeleo ya jamii, ni lazima kuwepo “Entropy” yaani kiwago cha vurugu ili kuweka mfumo mzuri. Hii imethibitika katika nchi zote zilizoendelea kifikra na kiuchumi duniani kama vile Marekani, Uingereza, Ujerumani, Japan, China, Ufaransa n.k. Nchi hizi bado zinaendelea na zitaendelea kutumia mfumo huu wa vurugu kujiletea maendeleo kwa kuvamia nchi nyingine inapobidi.

Kama ilivyo vurugu ktk kuhakikisha michanganyiko mizuri ya kisayansi, vurugu ktk vinchi vyetu maskini visivyo na viongozi bora na wenye maadili, ni kwa ajili ya kuwaunganisha watu ktk nia yao moja ya kujiletea ukombozi wa kweli wa kifikra na kiuchumi. Siku zote ukumbuke kwamba huwezi kumnyang’anya Simba nyama kwa kumpigia kelele tu bila kumfanyia vurugu labda awe ameshiba.

Wanasiasa ktk vinchi hivi ninawafananisha na “Vichochezi” yaani “Catalysts” ktk michanganyiko ya kisayansi. Hawa ni wa msingi sana maana wanaharakisha mchanganyiko na ndo wakorogaji. Ili wafanikiwe ni lazima wakubali wazi kwamba wao ni wachochezi ktk safari ya jamii kuelekea ukombozi wa kifikira na kiuchumi. Wachochezi hawa waelewe kwamba Simba ana tabia ya kuendelea kula nyama wawapo mbwa mwitu au Fisi watatu na hata mara nyingine kuwajeruhi lakini Simba ujipima uwezo na kuachia mzoga wawapo mbwa mwitu au Fisi ishirini pasipo hata mahitaji ya vurugu.

Nikiamini mifano imetosha, ni wazi sasa unaelewa mtu yeyote mwenye nia ya kuendelea kukukandamiza na kukuibia atakwambia wewe ni mtu mpole na mwenye amani kwa sababu anajua fika hutafika popote kwa njia hii. Viongozi wa vinchi hivi vidogo wanapigiwa wimbo huu na mataifa makubwa na wenyewe wana duplicate kwa maksudi kwa wanajamii.

Vinchi hivi maskini tumefika hapa tulipo kwa sababu tumerithishwa huu umaskini na ujinga wa kuitwa watu wenye amani wakati tuna imani tu kwamba iko siku watatenda. Amani hii imetufanya kuwa mbumbumbu kiasi kwamba kila mtu anatuibia kwa kupitia imani tuliyorithishwa pasipo kuelewa undani wake.

Inasikitisha kwamba watu wengi ktk vinchi hivi maskini ni “Madebe Matupu” yakijazwa yanaacha kuvuma. Simama uhesabiwe kama mpenda maendeleo wa ukweli, uongee, upambane si kwa nguvu ya njaa bali kwa nguvu ya upendo kwa wasionacho.

……Kama hujaielewa nia yangu njema ni kwa sababu una uvivu au mapungufu ya kuwaza, hivyo ninapokea kwa upendo mashambulizi yako…….

To be cont’d……
 
Philosophy uliyotumia ina mantiki na inakidhi muktadha katika kushabihiana na uhalisia wa mtanzania katika kupengenyua uchakachuaji
 
mkuu umeeleweka sana.
vyote vinakuwepo ktk harakati za mabadiliko.
 
Mkuu umetumia kiswahili cha kuzunguka sana. Ila binafs nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…