Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 27
Nawaza kwamba mfumo wa Elimu ya msingi hapa Tanzania unashida.
Unahitaji marekebisho makubwa.
Exaud,
Mawazo yako ni ya msingi
Sioni juhudi zinazofanywa kuifanya elimu ya msingi kuwa msingi.
,,,
WADAU wa Elimu mnasemaje?
EMMA,
Sasa nini kfanyike?
Waalimu na wanaharakati tutoeni hapa.
Mwalimu Nyerere alishatuwekea msingi wa nadharia itakayotumika katika elimu yetu. Tunaweza kutumia nadharia ya Elimu ya Kujitegemea kukiwa na marekebisho kufuatana na mapungufu tuliyoyaona wakati ule wa kutekeleza nadharia hiyo, pamoja na kuzingatia mabadiliko ya wakati wa sasa.
KITIA,
Ukipendekeza suala la Elimu ya kujitegemea, utapata upinzani mkubwa.
Elimu ya kujitegemea ilionekana kushindwa enzi za Nyerere.
Mkuu, hapo ndipo nilipokuwa ninalenga. Tuangalie maana/dhana ya Elimu ya Kujitegemea na madhumuni yake, tuone ni vipi ilishindwa, na katika kushindwa huko ni vipi ambavyo tutaweza kubuni mfumo na utekelezaji mzuri wa elimu ya msingi ambayo itakuwa na manufaa kwa wanafunzi na taifa kwa ujumla.
Je hii ndiyo Elimu ya MSINGI kweli?Wanafunzi wa darasa la saba kutoka Mbagala Kuu jijini Dar es salaam wakiwa katika mitihani yao ya kila mwezi.
Huu ndio mfumo wetu. Kaazi kweli kweli
Ni mawazo mazuri sana, lakini yanakosa vivid evidences,
Cha msingi walimu wathaminiwe na kulipwa maslahi mazuri tutaanza kuona matunda mazuri ya watoto wetu.Pia walimu wasichululiwe wale wanafunzi waliofeli tu bali hata waliofaulu vizuri.
Hali hii haiwezi kubadilika kwa sababu watoto wa wakubwa hawamo humu na fedha ambazo zingetumika kununua madawati zimefisadiwa na wakubwa hao ambao watoto wao wanasoma majuu.
tuungane tumwombe Mungu vinginevyo utumwa unarudi kwa kasi ya ajabu