Methamphetamine ya KSh Bilioni 8.2 Yaharibiwa Mombasa

Ikariiah

Senior Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
143
Reaction score
260
Your browser is not able to display this video.

Zaidi ya tani 1 ya methamphetamine yenye thamani inayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 8.2 imeharibiwa Mombasa leo, baada ya kukamatwa katika operesheni ya pamoja baharini mwaka jana.

Mizigo hio takriban kilo 1,036 ilikamatwa kutoka kwa chombo kilichokuwa baharini takriban kilomita 630 mashariki mwa Mombasa mnamo Oktoba 2025. Operesheni hiyo ilihusisha vyombo mbalimbali vya usalama, ikiwemo Jeshi la majini Kenya Navy na Kenya Coast Guard Service.
Your browser is not able to display this video.


Leo, maafisa wa usalama wamekusanyika katika eneo la Bamburi, Mombasa, wakiongozwa na Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen kushuhudia uteketezaji wa shehena hiyo.
Your browser is not able to display this video.


Lakini kwa nini inaharibiwa wakati kesi bado iko mahakamani?

Mzigo huo umehusishwa na kesi ya usafirishaji wa dawa za kulevya inayowakabili washukiwa 6 wa Iran katika Mahakama ya Shanzu, Mombasa. Kesi hiyo bado inaendelea, na mahakama tayari imeamua kwamba washtakiwa wana kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha mashahidi.

Kwa hiyo, uharibifu wa mzigo huo haupaswi kuchukuliwa kama hukumu ya mwisho dhidi ya washtakiwa. Ni hatua inayohusu mzigo uliokamatwa, huku mchakato wa mahakama ukiendelea.

Kukamatwa kwa mzigo huu pia kunaweka pwani ya Kenya na njia za baharini za Bahari ya Hindi katika 'spotlight' ya vita dhidi ya usafirishaji wa dawa za kulevya kimataifa. Waziri Murkomen amesema operesheni hiyo ilihusisha ushirikiano wa kitaifa na kimataifa katika kufuatilia chombo hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…