Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Amefanya assist ngapi???
Akipiga pasi tatu za goli na kuanzisha mashambulizi mengine matatu,Lionel Messi ameiongoza Argentina kuisambaratisha Paraguay 6-1 katika nusu fainali ya Copa America. Messi,akicheza kama kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Tata Martino,alikuwa kwenye kiwango bora alfajiri ya leo.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Angel Di Maria aliyefunga mawili na moja moja toka kwa Javier Pastore,Marcos Royo,Aguero na Higuain.
Messi sasa kama Nahodha ameiongoza Argentina kucheza fainali ya pili mfululizo baada ya ile ya Kombe la Dunia ambapo Argentina ilifungwa bao moja kwa bila na Ujerumani. Fainali ya Copa America itachezwa Jumamosi baina ya wenyeji Chile na Argentina. Mara ya mwisho Argentina kutwaa ubingwa ilikuwa ni 1993.
Tatu za moja kwa moja,tatu za kuzianza
Hivi ana magoli mangapi
Amefunga goli moja. Martino anamchezesha kama kiungo