Ruhazwe JR
JF-Expert Member
- Jan 31, 2011
- 3,402
- 944
Wote ambao hampendi kupokea ujumbe huu, mnaweza kuuzuia kwa kutuma neno STOP ALL (kwa herufi kubwa) kwenda #15622
unatuma neno STOP ALL (kwa herufi kubwa) kwenda #15622
Habari zenu wadau wa jamiiforums,
Leo bila ya woga naomba niseme yaliyonikuta: bila ya kujali wepesi au uzito wa suala hili.
Kuna SMS imeingia kwenye simu yangu ya mkononi nayo ipo hivi;
Sender:CCM
'CCM ipo imara. Watanzania tusikubali kuweka rehani umoja na amani ya nchi yetu'
Hii message imetumwa kwa malengo gani? TCRA inaruhusu masuala kama haya? Naomba nieleweshwe kwa wanaoelewa haya maswala vizuri.
Hebu tuelekeze vizuri, ukituma neno hilo "STOP ALL" siitafungia na simu zingine zenye umuhimu?
Enhe Preta!Nieleze namna ya kublock hizo msg toka kwa chama cha malori maana sitaki kupokea hata mesg moja.hiyo msg hata mimi niliipata....tena sio moja....zilikuwa zinaingia kama mvua.....nimeghadhibika sana....ikabidi nipige huduma kwa wateja wakanieleza jinsi ya kublock.....ni upuuzi mkubwa sana.....
Habari zenu wadau wa jamiiforums,
Leo bila ya woga naomba niseme yaliyonikuta: bila ya kujali wepesi au uzito wa suala hili.
Kuna SMS imeingia kwenye simu yangu ya mkononi nayo ipo hivi;
Sender:CCM
'CCM ipo imara. Watanzania tusikubali kuweka rehani umoja na amani ya nchi yetu'
Hii message imetumwa kwa malengo gani? TCRA inaruhusu masuala kama haya? Naomba nieleweshwe kwa wanaoelewa haya maswala vizuri.
Mkuu umesahau kwamba na mahakama zote za Tz zinapokea maagizo toka ofisi ya ccm lumumba? Angalia hukumu isije ikatoka ukatakiwa na kulipia gharama zote za uendeshaji wa kesi kama yaliyompata mheshimiwa Mpendazoe.Ikitumwa kwangu nawapeleka mahakamani.
TCRA na CCM ni kama vile chupi na makalio kwani havitengamani, kumbuka wakati wa uchaguzi kulikuwa na message nyingi sana za namna hiyo na watu wakalalamika saaana lakini hakuna ufafanuzi wowote toka TCRA mpaka leo hii, Sijui tuwatukanie nini ili wajue watu hatupendi huo mchezo wao
Waambie wakutumie wewehy massage ina ubaya gani? Kama ujumbe huutaki c ukae kimya?,hulazimishwi.