Mengine ya Upinzani yana Ukweli... Polisi wanatumiwa


Kuna Polisi ambae ni CCM na Chadema? funguka kidogo, usiwe punguani.
 
Nadhani serikali ya ccm ndiyo serikali inayoongoza Afrika kama sio duniani kwa kuweka mfukoni na kila mwenye fedha. Mambo yataendelea hivi mpaka lini? Mabadiliko ni lazima ili kuweka utawala utakaoheshimu sheria na usio dhaifu kama huu tulionao. Ningejisikia vizuri zaidi kama mtoa mada (Zomba) ndiye angekuwa amefikwa na madhila haya ili akome kutetea upumbavu wa serikali na vyombo vyake vya dola. Next time it might be you Zomba, mabadiliko ni lazima.
 

Zomba,leo ndio umeona polisi wabaya kwasababu ya kuwanyima haki ya msingi jamaa zako, wangelalamika wapinzani (cdm) ungewaponda
 
Si kila jambo lazima liwe ni la kisiasa bana! khaaaaa! Huo ni utendaji mmbovu wa hao ma ocd, ma rpc na sijui wengine. Kwani mmefuatilia huyo tajiri aliyemwaga pesa ili hawa wa-tz wenzetu wasitolewe ni wa chama gani???
Kisha kwanini wasichukuliwe hatua hao polisi wahusika kutokana na kukiuka sheria kwa maksudi kabisa. Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai unasema wazi kabisa mtuhumiwa lazima apelekwe mahakamani ndani ya muda wa saa 24. Hasa kama mtuhumiwa hajawekewa zamana. Kumhamisha tu haitoshi labda wamshushe cheo maana ataenda kuongoza sehemu nyingine na kuwafanyia watanzania wenzetu tena ufisadi huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…