Member wa Jf hawashidwi!!!!

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,442
Reaction score
8,695
Ukiwa kama member wa JF basi kaa ukijua ww ni mtu wa level tofauti na Social Media nyingine


#:Main topic! naomba ufafanuzi kwenye hizi point zangu tatu (3).

#: kwanini asilimia 85% ya walioajiliwa hali yao huku mitaani ni taabani,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,baada ya kupokea kiinua mgongo ndio wanatamba mjini.

#: kwanini baadhi ya wafanya biashara hali zao za kimaisha zinalingana hawafiki mbali kimaendeleo lakini wengi wapo level moja.


#: unazania kuweka akiba ndio njia sahihi ya kufikia malengo??




Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamani jaman jaman tutafute pesa wadau oohoooooo!
 
Dr. Shika anasema vp kwani?

"Honesty is very expensive gift. Do not expect it from cheap people" mjr95.

 
Hilo la kwanza ni kawaida kwamba mianya ya hela za bure imezibwa pia huu msemo 'masikini akipata matako hulia mbwata", hiyo ni kuelezea hoja ya kustaafu ukapewa milioni kadhaa na huna malengo nazo.

Mbili huwezi generalize kwani mfanyabiashara kama Dewji,Bhakhresa,Mengi na wengine wengi ni wakubwa sana na huwezi walinganisha na kina mimi. Ambaye hata leseni ya biashara,uvuvi na tra siwezi lipa nafanya kwa magendo unafikiria nini hapo(brainstorm)

Mwisho kwanza ni unadhani sio "unazani" Kama una malengo jibu ni ndio na kinyume chake.
 
#: unazania kuweka akiba ndio njia sahihi ya kufikia malengo??




Sent using Jamii Forums mobile app


Nimechagua kuchangia ktk hilo hapo.

Kuweka akiba ni jambo jema sana na nila lazima kufanya wakati wote kadri itakavyowezekana.

Wengine huamua kuweka akiba kwa aina inayofanana na kulipa kodi. Kwa mfano kila anapopata fedha basi anakata asilimia fulani kama anavyokatwa kwaajili ya kodi na kiasi hicho kinaenda kwenye akiba.

Tofauti inakuja kwenye malengo ya hiyo akiba na aina ya uwekaji, hata hivyo kuweka akiba bila kujali aina ya uwekaji kuna manufaa kuliko kutokuweka akiba;

1. Kama una chanzo cha kuzalisha mapato na sehemu ya faida ukaweka akiba ukijipangia malengo kuwa ikifika kiasi fulani ufanye jambo fulani. Ni imani yangu utafanikiwa malengo yako.

2. Wengine hupata kiwango kikubwa cha fedha na wanakua hawajajipanga bado kuzifanyia shughuli fulani. Hivyo unaweza kuziweka akiba kwa mtazamo unaofanana na uwekezaji, kwamba unaziweka benki na kuwaambia kila baada ya muda fulani, riba (faida) utakayolipwa na benki kwa kipindi hicho uichukue kwa matumizi. Kuna uwezekano wa kutimiza malengo yako utakapokuja kuyapanga hapo baadae maana fedha hiyo itakua salama.

3. Kuweka akiba isiyoongeza thamani ya kiwango cha fedha uliyoiweka inaweza sababisha usifikie malengo yako hasa kwenye mazingira kama ya nchi yetu ambayo thamani ya shilingi inaporomoka kadri siku zinavyoenda.
Maana yake kwa mfano, mwaka 2005 uliweka akiba isiyoongeza thamani (kwy kibubu au chini ya godoro) kiasi cha shilingi milioni moja kwa lengo la baada ya miaka saba uje kumpatia mdogo wako kama kianzio cha biashara ya bodaboda na kwa wakati huo pikipiki ilikua ikiuzwa laki saba.
Kutokana na fedha kushuka thamani, baada ya hiyo miaka saba bei ya pikipiki inakua milioni moja na laki tatu. Ni wazi hutafikia malengo.

Imetosha kwa leo nisikuchoshe maana naandika kwa kutumia tekno nisije kuharibu mtiririko nikapoteza maana ya nilicho kikusudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…