Mdaiwa hafungwi

Arsenal

Senior Member
Joined
Aug 12, 2008
Posts
190
Reaction score
71
guys,

Jana nilipata bahati ya kwenda mahakama ya ilala pale lumumba katika issue za kesi yangu moja ivi ya barabarani nikakuta watu wenye kesi za madai jinsi wanvotaabika utadhani wao ndo wametapeli kumbe wao ndo wametapeliwa, PP anawaambia kwa umeongea na mdaiwa?? mkae chini akulipe koz apa mahakamani mdaiwa hafungwi!!!anaweza kukulipa akiamua shillingi elfu tano kila mwezi na hakimu akakubali na kesi ikafungwa!!!!jamani!!!!watu wanamjibu mdaiwa hapokei simuuuuu!!!na anajua kwamba hafungwi please tusaidie!!!ilikuwa na huruma mpaka mwisho!! mi naona serikali ingeweka sheria kwamba ikithibitika umekopa au tapeli basi ufungwe angalau mwaka 1 then ukitoka umalizane na anaekudai ukishindwa unamalizia miaka 4 ivi apo ndo utapeli utaisha mjini apa na ata banks zitapunguza masharti ya kukopesha watanzania wenye nia ya kulipa lakini hawana dhamana inayoridhisha..
thats my take...mnaonaje wana jf??
 
Ni kweli kesi ya Madai huwa ni ngumu sana, ndio maana mara nyingi kwa anayejua huwa anafungua kesi ya "Wizi wa Kuaminiwa"

Lakini hata hiyo pia, mtuhumiwa anaweza kukiri kosa na akaomba kulipa kwa awamu...

Sheria hizi bwana!!
 
Yani, ukope bank, usilipe, then wakishakufunga ndo hela yao itarudi?? ndo maana kesi ya madai hukumu ni kulipa kulingana na kiasi unachopata wakati huo, unaweza kudaiwa 10m, lakini una uwezo wa kulipa 2,500 kila mwezi kulingana na kipato chako na ikawa hivyo!!
 
Jamani, mdaiwa anaweza kufungwa ili mradi wewe mdai uwe tayari kuilipa magereza "ada za kukaa na huyo mdaiwa" mpaka hapo atakapo kulipa, msijidangaye kuwa mdaiwa hafungwi !!!!!
 
Jamani, mdaiwa anaweza kufungwa ili mradi wewe mdai uwe tayari kuilipa magereza "ada za kukaa na huyo mdaiwa" mpaka hapo atakapo kulipa, msijidangaye kuwa mdaiwa hafungwi !!!!!

You nailed it home buddy, and it is provided for under Civil Procedures Code that the judgement debtor may be committed to a civil prison ila ndo huwe na fweza ya kumlisha mapocho pocho!
 
Jamani, mdaiwa anaweza kufungwa ili mradi wewe mdai uwe tayari kuilipa magereza "ada za kukaa na huyo mdaiwa" mpaka hapo atakapo kulipa, msijidangaye kuwa mdaiwa hafungwi !!!!!
kifungu hicho kipo, lakini kumbukumbu za mahakama zinaonyesha kesi zilizoamuliwa kwa kifungu hicho ni sawa na 0.002% hivi,

Yani wewe unanidai, then unatoa hela tena nikale maharage na ugali bure, na kodi ya jengo unanilipia?! (busara kwa wadai) sio wa wadai kama akina Masaweee!!
 

Hela yenyewe sio nyingi nadhani ya juu itakuwa shs 500 kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…