Anahitajika dada wa kazi za nyumbani, majukumu yake ni kama yafuatayo:-
- Kufanya usafi wa nyumba, kufua, kudeki, kuosha vyombo
- Kupika
- Kucheza na watoto
Ujuzi
- Elimu ya msingi, sekondari au ualimu wa chekechea
- Awe ni mtu anayependa usafi, kwake mwenyewe pamoja na mazingira yanayomzunguka.
Malipo
- Mshahara kwa mwezi 100,000/=
- Matibabu bure
- Kula kulala bure
Muda wa mkataba
- Miezi miwili, kwa sababu aliyepo anaenda mapumzikoni
Faida zingine
- Kama atakuwa mcheshi, mtu wa kujituma na kujifunza vitu vipya; baada ya mkataba anaweza kuendelezwa na kufanya kazi zingine
Kama upo mkoa wa kilimanjaro au Arusha, itakuwa vizuri zaidi; kwa sababu eneo la kazi ni Arusha.