GE2025 Mchungaji Arusha amwombea Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Mchungaji Samweli Karao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ngaramtoni mkoani Arusha, ameendesha maombi maalum Julai 23, 2025 kwa ajili ya viongozi wa CHADEMA, akimjumuisha Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu.

Katika maombi hayo, Mchungaji Karao alimuomba Mwenyezimungu ampe Lissu wepesi wa kutoka kizuizini, huku akituma salamu maalum kwa kiongozi huyo ambaye kwa sasa yuko gerezani. Akizungumza mbele ya waumini na viongozi wa CHADEMA mchungaji huyo alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kufikisha salamu zake kwa Lissu, huku akitamka kwa imani maneno haya: "Neema ya Mungu imfunike." Maombi hayo yalifanyika mara baada ya ibada ya kuvunja tanga kufuatia maziko ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel.

Your browser is not able to display this video.
 
Mchungaji Samweli Karao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ngaramtoni mkoani Arusha, ameendesha maombi maalum Julai 23, 2025 kwa ajili ya viongozi wa CHADEMA, akimjumuisha Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu.

Katika maombi hayo, Mchungaji Karao alimuomba Mwenyezi Mungu ampe Lissu wepesi wa kutoka kizuizini, huku akituma salamu maalum kwa kiongozi huyo ambaye kwa sasa yuko gerezani.

Akizungumza mbele ya waumini na viongozi wa CHADEMA mchungaji huyo alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kufikisha salamu zake kwa Lissu, huku akitamka kwa imani maneno haya: "Neema ya Mungu imfunike."

Maombi hayo yalifanyika mara baada ya ibada ya kuvunja tanga kufuatia maziko ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…