Mbunge amtunishia msuli DC!

sir.JAPHET

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2012
Posts
699
Reaction score
137
*Ni Sugu wa Mbeya Mjini, akimbia ukumbini
*DC asema adhabu yake ni kumpuuza tu

MKUTANO wa kutangaza matokeo ya darasa la saba Mkoa wa Mbeya, nusura yaingia doa, baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, kupitia (CHADEMA) kulumbana hadharani na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela.

Hayo yaliibuka jana, baada ya kikao hicho cha kutangaza matokeo hayo ambacho kilikuwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Maria Mtunguja.

Mbilinyi alifikia uwamuzi huo, baada ya DC Meela kutoa sababu za kuchelewa kwa ujenzi wa madarasa katika Kata ya Kiwira, akidai umesababishwa na viongozi wa CHADEMA.

"Kuchelewa kwa ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari na kukosa madarasa wakati kuna wanafunzi wanahitaji kutumia madarasa hayo kuanzia Januari, mwakani (mwaka huu) ni uzembe unaosababishwa na viongozi wa CHADEMA.

"Kukwama huku kunasababishwa na wananchi wa Kata ya Kiwira, kuambiwa na diwani wao, Laulent Mwakalebule (CHADEMA), kuwa wachangie Sh 3,000 kwa kila mwananchi kiasi ambacho hakitoshi kukamilisha ujenzi kutokana na idadi ya wananchi wa kata hiyo kuwa ndogo," alisema Meela.

Bila wasiwasi DC Meela alimtupia shutuma moja kwa moja Mbilinyi kuwa akawaeleze viongozi wenzake na wanachama wake, waache kuingiza siasa katika shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake, Mbilinyi akijibu kauli ya DC Meela, alisema katika jimbo lake lina kata 18, zinazosimamiwa na CHADEMA na maendeleo yapo.

"Namwambia DC aache kujiingiza kwenye siasa na fanyeni kazi za maendeleo ili kujenga madarasa ya wanafunzi ili waweze kuanza masomo," alisema Mbilinyi.

Lakini katika hali ya ajabu, ghafla Mbilinyi alimtolea lugha chafu ambayo hatuwezi kuiandika gazetini, kutoka nje ya chumba cha mkutano, kitendo ambacho kilionekana kuwashangaza watu waliokuwapo ukumbini.

Kikao hicho kilikuwa na wabunge, maafisa tawala wa wilaya zote za Mkoa wa Mbeya, maofisa elimu wa wilaya na afisa elimu wa Mkoa.

Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo, walitaka mkutano huo uvunjwe, lakini wengine waliomba uendelee na kusema si kitendo kizuri mtu mmoja asababishe mkutano uvunjike.

Baada ya malumbano hayo, DC Meela alisema adhabu ya mtu kama huyo ni kumpuuza na kumwacha, kwa sababu hajui nini anachokifanya.

"Ndugu zangu mtu mmoja kama Mbilinyi, adhabu yake ni kumpuuza tu, tuendelee kujadili mambo ya msingi kwanza, tuone ni namna gani vijana wetu wataingia darasa la kwanza na wale wa kidato cha kwanza.

"Naamini kuna baadhi ya shule katika halmashauri mbalimbali, hazijakamilisha madarasa na asilimia kubwa ya shule hizi, zitakamilika mwishoni mwa Januari na wanafunzi wataanza masomo yao mwanzoni mwa Februari mwaka huu," alisema Meela.
 
Hicho kikao inaonekana kilikuwa na mengi zaidi ya yaliyoandikwa hapo kwa akili ya kawaida haiwezekana maneno ya kurushiana watu wawili watu wote watake mkutano uvunjwe, Je nikwanini Sugu alipotoka mkutano uktaka uvunjwe ? kwanini tusiamini kuwa SUgu alikuwa na hoja then ilipokataliwa ndo akatoka?
 
Kama hali ni mbaya kiasi hiki;Kwa nn serikali isichukue mabilion yake wanayowadai waliokopa kutoka kwao?

Mbunge Khamis Kigwangalah(Nzega) na Mbunge Mstaafu Christant Majiyatanga Mzindikaya(Kwela) yale mabilion yetu waliyokopa kuwa watafufua zao la Pamba(Tabora) na wataanzisha kiwanda cha nyama na maziwa (Rukwa) WALIKWISHA TURUDISHIA?

Haya mambo ya kuchangishana ili hali serikali haionyeshi juhudi zozote kurudisha mabilion yaliyofichwa Uswisi na kisiwani(Chenge)kwa njia za rushwa na vigogo hayakubaliki!

MBUNGE Sugu is absolute right kukataa michango hii!
 
Hawa watawala wamechanganyikiwa,mnawaambia watu wachangie,ujenzi ukikamilika mnasema serikali imejenga.ACHENI WIZI KUSANYENI KODI MFANYE KAZI ZA MAENDELEO.(kodi zetu mjengee mahekalu sisi haohao tuchangie ujenzi wa shule).ni upuuzi.
 
Acha kudanganya watu kuwa hii habari ni ya jana, wakati tukio lina karibia wiki ya pili na hapa jf lilisharipotiwa kitambo...jirekebishe.!
 

Kaka tafadhali pambanua na kuanzisha thread mpya ili Kigwagwangala aka mzee wa Vitumbua aje aji u tuhuma maana yumo humu jf.
 
safi sana SUGU, nakujua una kitu flani ambacho watu wengi hawana, nacho ni kusimamia kile unachokiamani, , na kiongozi mzuri lazima uwe na hiyo characteristic.
 

kama unauhakika na unachokiongea fungua uzi wake wadau wadadavue.!
 
Haya mambo yanawezekana Tanzania tu. Kila kukicha walalahoi wanalipishwa kodi, vigogo wanapeta na ufisadi. Mlalahoi huyo huyo unamchangisha wakati vigogo wanakwapua na kukimbizia Uswis.


NAPINGA KWA NGUVU ZOTE DHANA YA KUCHANGISHA WALALAHOI.
 
Ni aibu nchi inayomiliki ndege ya rais na magari ya milioni 200 kwa zaidi ya wakuu wa wilaya 200 wakuu wa mikoa 27 na viongozi mbalimbali ni haki alivyowatukana huyo mkuu wa wilaya gari lake matumizi ya mafuta na matengenezo kwa mwaka ni ni madarasa 5
 
Hua nikizipitiga nyimbo zake nafarijika na ham hua hainiishi,huyu jamaa harakati amezianza siku nyingi tangu za kugoma kusimama anakwambia ntakaaje wakati nimesimama bwana?anakwambia itafikia kipind pingu tutazioa kama bangili nk.kazi ya kujenga nyumba za wananch ni za selikali tuliyo ipa dhamana maana wanachukua kod zetu tununuapo kila kitu.ccm uongowenu tulisha ujua na tunajua hamuwez kubadilika maana mmesha zoea wewe mzee wa miaka hamsini anaweza acha tabia yake ya kuroga? Mkinyooshwa mtavunjika kwahivyo ondokeni tu na 2013 mtavalishwa gwanda tujue hiyo 2015 atakae baki ccm ninani. Juzi kaya 150 huko meru zilihamia cdm baada ya kujua kaz ya kujenga shule ni ya selikali.eth tujenge zahanati!! Hiyo tra inakaz gani?eura je?nk
 
Kaka tafadhali pambanua na kuanzisha thread mpya ili Kigwagwangala aka mzee wa Vitumbua aje aji u tuhuma maana yumo humu jf.

Nakumbuka MB KIGWANGALLAH aliwahi kuulizwa na kambi ya Bashe swali hilo akiwa Tabora!Nina uhakika wa asilimia zote kuwa hawa wabunge walikopa mabilion lkn sijui kama walilipa au la!

Lkn hadi katikati ya mwaka wa jana Kigwangwallah alipobanwa na kambi ya Bashe aliwahi sema wazi kuwa YY NA WENZAKE WALIOKOPA KUFUFUA ZAO LA PAMBA TABORA HAWAJALIPA BADO HILO DENI;Labda kama walilipa baadae!
 
kama unauhakika na unachokiongea fungua uzi wake wadau wadadavue.!

Nina uhakika wa asilimia zote 100 kuwa WABUNGE HAWA WALIKOPA MABILION YETU;Lkn sina uhakika kama walilipa au la!Wenyewe ndiyo wanaweza jibu sawia!
 
Ni udhaifu wa viongozi wetu kila wanaposhindwa na kuishia kutoa visingizio vya wapinzani! kukosolewa ni sehemu ya maendeleo na kioo cha kupijima wapi umekosea na kujisahihisha.
 
Kampuni namba 13 ni ya Kigwangwallah na wenzake;kama hali ni mbaya na wao kama hawajatulipa si watulipe sasa
 
3000 ndogo????aache upuuzi uyo,mbona sie tunalip 2500(Tunduma) na bd maendeleo yameonekana???wamekalia wizi tu hao,kama wanaubavu watoe report ya mapato na matumizi!!!😱😡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…