Mbegu za maboga huongeza nguvu za kiume, soma faida kiafya za kutumia mbegu za maboga

lil_nocran

Member
Jul 10, 2014
46
18
MBEGU ZA MABOGA HUONGEZA NGUVU ZA KIUME,SOMA FAIDA KIAFYA ZA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA.

Mbegu za maboga zina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Mbegu za maboga zimethibitika kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya aina mbalimbali kuanzia magnesium, manganese, shaba, protini, zinki nakadhalika. Zifuatazo ni baadhi ya faida za matumizi ya mbegu za maboga.

1.KuongezaMaziwa Kwa Wanawake Wanao Nyonyesha : Kwa wanawake wanao nyonyesha matumizi ya mbegu za maboga huwasaidia kuongeza kiwango cha maziwa yenye afya kwa watoto wanao nyonya.

2.Mbeguza maboga zina kiwango kikubwa cha madini ya magnesium ambacho mwanadamu anatakiwa kukitumia kila siku.

3.Mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha madini ya zinc ambayo yana faida mbalimbali katika mwili wa mwanadamu kama vile kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha uwezo wa kuonja na kunusa, ukuaji wa seli mbalimbali za mwilini, kuimarisha afya ya macho na ngozi, kulinda na kuimarisha insulin pamoja na kuongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa wanaume.

4.Mbeguza maboga ni miongoni mwa vyanzo bora kabisa vya mafuta na acid zitokanazo na mimea ambazo zina faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu.

5.Mbeguza maboga zinasaidia katika kulinda na kuimarisha ufanisi wa tezi kwa wanaume

6.Mbegu za maboga zina faida kubwa sana kwa wagonjwa wa kisukari kwani zinasaidia katika kulinda, kuboresha, kuimarisha na kurutubisha insulin

7.Mbeguza maboga zina imarisha na kulinda afya ya moyo na ini

8.Mbeguza maboga zinasaidia katika kuboresha usingizi. Kama una matatizo ya usingizi unashauriwa kutafuna mbegu za maboga pamoja na tunda kidogo. Hii itakusaidia katika kupata usingizi mzuri.

Anza kujenga tabia ya kuwa unatumia mbegu za maboga kwa faida mbalimbali kwa afya ya mwili wako kama ilivyo onyeshwa hapo juu. Kwa anaehitaji mbegu wasiliana na simu,

Sms 0689095488
 
Hizi mbegu ni shida tupu,kuna kipindi fulani nilikuwa nazitumia kwa fujooo,kilichofuata bwana Abdalla kichwa wazi anasimamisha turubai kwa ghadhabu anataka haki yake kila wakati.
 
sasa ngoja nianze kilimo cha maboga...n
hii ni fursa ya kupiga hela tena kama kile kipindi cha mayai ya kwale
 
siku izi kasi ya propaganda za mayaiya kwale zimepungua sana. something must be wrong somewhere...
 
vs

Wale wa supu ya pweza kazi kwenu

Wakulima tunzeni na mlinde mashamba yenu kabla vita haijaanza

45e214ba68092df18e31c49f5ace360b.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom