Wakati tunaingia mwaka wa 3 wa utawala wa awamu ya 5, inanikumbusha hadithi nilizosimuliwa na mabibi siku nyingi kuhusu kijana jasiri wa Kisukuma. (Mimi sio msukuma) Nafikiri pia unaweza kuipata hadithi hii kwenye vitabu katika lugha nyingi.
Kuna hadithi moja ya Kiingereza ipo mtandaoni inayofana kidogo na hii. Katika hadithi hiyo huyu kijana anaitwa Masala Kulangwa. Mimi sikumbuki jina lake wakati ninasimuliwa kwa hiyo nitatumia jina linalokaribiana na hili - Massalu. Mpaka leo naukumbuka wimbo wa hadithi hii bali sitaunukuu kwa sababu Kisukuma changu ni karibu na sifuri.
Title ya wimbo ni:
Mayo, Mayo Nabhulaga Shing'weng'we ikimaanisha
Mama, Mama Nimemuua Shing'weng'we
(Hapa pia sijui kama nimekikosea hicho Kisukuma. Watani zangu sahihisheni.)
Ni hadithi ya kijana jasiri aliepitia mengi ili aiokoe jamii yake. Wengi walifurahia kuokolewa kwao lakini kuna wachache walichukizwa. Nitakuachia msomaji uone kama kuna ushabihiano kati ya kijana Massalu Kulangwa na uongozi wa awamu ya 5.
Kama huoni ushabihiano, ichukulie tu kama bed-time story. Wasomeeni watoto wenu hadithi wakati wa kulala. Ni bora kuliko kuangalia katuni.
MAYO, MAYO NABHULAGA SHING'WENG'WE
PAUKWA......hapa mnaitikia PAKAWA.
au
HADITHI HADITHI.........basi nyie mnaitikia HADITHI NJOO, UTAMU KOLEA.
Hapo zamani za kale palikua na himaya moja iliokuwa na watu wengi sana, wanyama wengi (mifugo na wa porini), neema ya vyakula na watu wenye furaha sana.
Sasa siku moja Mfalme aliwatuma wawindaji wake waende porini wakalete wanyama mwitu kwa ajili ya karamu yake kwa sababu alikua amechoka kula ng'ombe, mbuzi, kuku na BATA. Lakini isivyokuwa kawaida yao wale wawindaji hawakurudi. Mfalme alikasirika sana na kuahidi kuwapa adhabu kali watakaporudi.
Ilipofika asubuhi siku ya pili akatuma kundi jingine la wawindaji kwenda kuleta wanyama na kuwaleta wale wenzao waliotumwa jana yake. Lakini, kama ilivyotokea jana yake, wale wawindaji pia hawakurudi.
Siku ya tatu Mfalme akasema safari hii nitakwenda mwenyewe pamoja na mashujaha wangu mahiri nikalete wanyama pori kwa ajili ya karamu yangu. Lakini mpaka giza linaingia, Mfalme pamoja na mashujaha wake wakawa hawajarudi.
Watu wakaanza kuhamaki. Hakuna mtu mwengine aliejaribu kwenda tena msituni.
Hii haikusaidia kitu kwa sababu, siku moja asubuhi watu waliamka na walipofungua milango yao; HAMAD, mbele yao wakaliona ZIMWI moja kubwa sana katikati ya mji wao.
Watu walianza kukimbia huko na kule, mifugo nayo ikawa inakimbia hovyo hovyo. Wakati wote huu lile ZIMWI lilikua linameza chochote kile kilicho mkaribia. Wakati linameza hawa watu na mifugo lilikuwa linawaambia kuwa yeye ndie mfalme wao sasa na anaitwa Shing'weng'we.
Kwa siku kadhaa hivi hili li-Shing'weng'we liliendelea kumeza watu na mifugo ya mji wote mpaka ikawa hakuna kiumbe chochote tena kilichoonekana kutembea. Li-Shing'weng'we lilipoona hamna kitu cha kumeza tena likaondoka kwenda kutafuta mawindo mengine.
Wakati wote huu li-Shing'weng'we lilipokuwa linameza watu na mifugo, kuna mama mmoja aliekuwa mjaamzito. Huyu mama alijificha vizuri sana kwenye vichochoro kati ya nyasi na akakaa huko mpaka Shing'weng'we alipoondoka. Hili Zimwi halikwenda mbali sana na yule mama alikuwa analisikia mara kwa mara.
Yule mama akabaki tu pekeyake lakini Mungu-bariki aliweza kujifungua salama mtoto wa kiume. Huyu mama akampa mwanae jina la MASSALU KULANGWA.
Mama na mwana waliendelea vizuri na li-Shing'weng'we likawa halisikiki tena. Waliendelea hivi mpaka kijana akawa mkubwa. Siku zote hizi yule mama alimkanya mwanae Massalu asiende mwituni. Acheze tu pale mjini karibu yake. Massalu akamuuliza mama yake, "kwa nini mama, na mbona tupo peke yetu hapa mjini, baba yangu yupo wap?"
Kila huyu kijana alipokua anamuuliza mama yake yale maswali, yule mama alibubujikwa tu na machozi lakini hakuyajibu maswali yake. Alimwambia tu "mimi ni mama yako na ninakukanya usikanyage ndani ya ule msitu."
Yule kijana alivyoendelea kukua akamwambia mama yake; "kama hutaki kuniambia kilichopo mwituni basi nitakwenda nikakione mwenyewe." Mama alipoona yamefikia pale akaamua kumueleza Massalu kila kitu kilichotokea pale mjini kwao. Kuwa watu wote pamoja na baba yake na mifugo yote ilimezwa na ZIMWI moja katili sana linalojiita SHING'WENG'WE.
Kijana akadhamiria kwenda kuliua lile Zimwi. Mama alimsihi sana Massalu asiende. Alimwambia "wewe ndie mwanangu pekee, ndie msaidizi wangu, mamayako nazeeka sasa, ukimezwa na Shing'weng'we nani atakaenitunza?" Massalu akamwambi mama yake kuwa ni lazima akamtafute huyu Shing'weng'we na amuue.
Mama akawa ameshindwa sasa. Mama akamwambia Massalu kuwa atamruhusu kwenda isipokuwa atumie silaha na kinga atakayompa wakati wote. Alimpa Massalu silaha za marehemu baba yake, halafu akachukua kitu ghalani kwake na akakifunga kwenye kitambaa cheusi na kumvisha Massalu kwenye mkono wake wa kulia.
Massalu akauliza kile alichofungwa mkononi ni kitu gani. Mama yake akamwambia hiyo ndio kinga iliotuokoa wewe na mimi wakati Shing'weng'we alipokua anameza kila kitu. Hakumwambia ni kitu gani lakini alimuahidi kumwambi baada ya kumuua Shing'weng'we. Basi kila asubuhi Massalu alitoka na kuingia mwituni. Atakacho kiua alikimbia nacho nyumbani kumuonyesha mama yake. Kila aliporudi kuwinda alikuwa na furaha kuwa amemuua Shing'weng'we na aliimba Mayo, Mayo Nabhulaga Shing'weng'we au Mama, Mama Nimemuua Shing'weng'we
Siku ya KWANZA alikwenda na kuua mjusi. Akarudi akipiga yowe "Mayo, Mayo Nabhulaga Shing'weng'we" Mama yake akamwambia kuwa yule ni mjusi tu, li-Shing'weng'we ni likubwa sana mwanangu. Lakini asante mwanangu, ngoja tumchome huyu mjusi aongezee mboga zetu za leo.
Siku ya PILI alikwenda na kuua swala. Akarudi tena mbio na kuimba, "Mayo, Mayo Nabhulaga Shing'weng'we" Mama yake akamwambia kuwa yule ni swala, li-Shing'weng'we ni likubwa sana mwanangu. Lakini asante baba, ngoja tumpike huyu swala, atakuwa kitoeo chetu cha siku kadhaa.
Siku nyingi zilipita, kuna siku alileta kiboko, au faru, au twiga, mpaka tembo lakini mama akaendelea kumwambia mwanae kuwa hao sio li-Shing'weng'we. Sasa siku moja Massalu aliingia mwituni na kwenda mbali zaidi ya siku zingine. Kadri alivyokua akitembea alisikia ardhi inatetemeka. Kwa mbaali kidogo akaona pango kubwa sana. Na kadri alivyolisogelea lile pango lile tetemeko liliongezeka na sauti moja nzito ya ajabu ilisikika. Massalu aliendelea tu kulisogelea pango kinyemela huku akiwa ameshikilia silaha moja nzito ya marehemu baba yake kwenye ule mkono wake wa kulia aliovishwa ile kinga na mama yake.
Alipofika pangoni akaliona dubwana moja kubwa kupita kiasi. Lilikua limelala, ile sauti nzito na lile tetemeko la ardhi kumbe alikua anakoroma usingizini. Palepale Massalu akajua hili ndio li-Shing'weng'we. Basi alitumia ile silaha ya baba yake, na kwa nguvu zake zote akalipasua kichwa li-Shing'weng'we na kuliua.
Wakati anaangalia ni vipi atalibeba hili dubwana mpaka kwa mama yake akawa anasikia mayowe toka tumboni mwa Shing'weng'we. Basi akaamua kulipasua tumbo lake. Hapo hapo watu wote waliomezwa, pamoja na mifugo na wanyama pori wakatoka tumboni mwa Shing'weng'we.
Watu walishangilia baada ya Massalu kuwaelezea hadithi yote. Baba yake Massalu akamtambua mwanae kwa zile silaha alizokuwa anatumia. Mfalme nae akamshukuru sana na kumwambia Massalu atakuwa mshauri wake na kumuahidi ufalme siku sio nyingi kwa sababu Mfalme alikua amezeeka sasa.
Lakini kwa bahati mbaya wakati Massalu anakata tumbo la Shing'weng'we kuwaokoa watu, kuna bwana mmoja alikatwa sikio. Yule bwana alijitokeza na kumkabili Massalu. Akauliza; "iweje wenzangu wote uwatoe salama bali mimi unikate sikio langu. Ni lazima unilipe fidia." Watu wakamuuliza kwa nini hana shukrani, na ni fidia gani anayoitaka? Akasema kwamba na yeye ni lazima amkate Massalu sikio kama alivyokatwa yeye.
Watu wote walifadhaika sana na alichokitaka yule alijeruhiwa. Wakamshauri warudi mjini na huko Mfalme atatoa uamuzi wa mwisho. Waliporudi mjini kitu cha kwanza Massalu alichotaka kujua ni kile kilichomo kwenye ile kinga yake iliyofungwa na kitambaa cheusi.
Mama yake alimwambia kuwa; "nilipokua najifungua ujaauzito wako kitovu chako kiliizunguuka shingo yako na hukuweza kulia. Na hata nilipoweza kukiondoa kile kitovu Massalu mwanangu hukulia na nilifikiri umekufa. Lakini mara tu niliweza kukunyonyesha." Akaendelea kusema kuwa alipokikata kile kitovu hakukizika bali alikiweka juu ya jiko mpaka kilipokauka na kukihifadhi. Yule mama alijua kuwa isingekuwa kile kitovu Massalu angelia na kulifanya li-Shing'weng'we liwaone na kuwameza. Kile kitovu ndio ilikuwa kinga yao.
Baada ya siku tatu Mfalme aliwaita watu wote ili aje aamue ile kesi ya Massalu na yule mtu aliekatwa sikio.
Unadhani ni hukumu gani aliyoitoa Mfalme na kuafikiwa na watu wote?
THE END.
============================
Kuwasaidia watu na tafsiri ya hadithi hii, fikiria kuwa kila jipu ni Shing'weng'we.
TRA
TPA
Watumishi hewa
Vyeti feki
Madawa ya kulevya
Makinikia
Mikataba mibovu ya madini
Sheria kandamizi ya madini
Viongozi dhaifu
n.k.
Kila kimojawapo hapo kinaweza kuwa Shing'weng'we?