Maumivu ya kifua

Maumivu ya kifua

ntiluhungwa

Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
79
Reaction score
59
Naomba tujuzane kuhusu afya kwa ufupi

Kwakipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watu wanaokuja hospitalini wakilalamika kuhusu maumivu ya kifua pamoja na mgongo.

Zipo sababu nyingi sana zinazosababisha mtu kupata maumivu ya kifua na mgongo.
1.Heart attack....ni ugonjwa wa unaosababishwa na kufa kwa sehemu ya misuli ya moyo kutokana na kukosa damu yenye kiwango cha kutosha cha oksijeni.

DALILI ZA HEART ATTACK
Kuhisi mgandamizo kwenye kifua,kifua kubana,maumivu ya kifua,kuhisi misuli ya taya,shingo na mgongo kuwa inavuta.Kichefuchefu,tumbo kujaa gesi na maumivu ya tumbo,kutokupumua vizuri(kupumua nusu nusu), kutokwa na jasho wakati kuna baridi,uchovu,kichwa kuuma na kupata kizunguzungu. Uzionapo dalili hizo usizipuuze nenda hospitali mapema sana.

2. INDIGESTION

hili siyo tatizo ila ni kama alarm inayokueleza kuwa katika mwili wako kuna tatizo linaendelea.e.g Gastroesophageal reflux disease,ulcers au matatizo ya mfuko wa nyongo.Hii kitu inafanya tumbo linajaa gesi na baadae gesi hiyo hupanda juu kupitia oesophagus kusababisha kifua kuuma.

3. PANIC ATTACK
Mtu mwenye panic attack anakuwa na dalili kama za heart attack,panic attack ni tatizo la mtu kuwa na hofu kubwa kupita kiasi na wakati mwingine mtu huyo huwa anahisi kuwa anakufa na baada ya hapo mapigo ya moyo huenda kasi,kushindwa kupumua vizuri,kutokwa na jasho na kupata ngazi baadhi ya sehemu za mwili wake.N.B Panic attack sio ugonjwa ila ni matatizo ya kisaikolojia.

4.ANGINA

Not enough oxygen reaches the heart, causing chest pain(kiwango kidogo cha oksijeni kwenye moyo..mara nyingi hali hii husababishwa na damu iliyoganda kuziba misuli ya moyo.Angina pia ni dalili ya ugonjwa wa mishipa ya moyo inayoitwa artery(coronary artery disease).

5. Costochondritis is an inflammation ya makutaniop ya sternum na mbavu za juu za kifua,maumivu yanayosababishwa na costochondritis huwa ni localized na mara yingi maumivu yake hutokea sehemu ya juu ya kifua hasa unapobonyeza hiyo sehem au unapojinyosha kwakutanua kifua.Tatizo hili hutokea sana kwa mtu anayefanya kazi nzito kama vile kubeba mizigo mizito au kunyenyua chuma(gym).

6. Sinusitis is an inflammation or swelling of the tissue lining the sinuses.Tatizo hili hupelekea pua kuziba ingawa huna mafua na upumuaji huwa mbaya kwakuwa mtu mwenye tatizo hupumua kwakutumia mdomo.Nose congestion(yaani pua kuziba) hupelekea mtu kupata maumivu makali ya kifua na mgongo na wakati mwingine kifua huwa kizito sana.

Zipo sababu nyingi sana sinazosababisha kifua kuuma kwahiyo unapohisi kuumwa na kifua ni vema uende hosipitali kwaajili ya uchunguzi zaidi,maumivu ya kifua siyo ya kukaa nayo kwasababu huweza kukuletea shida kubwa zaidi inayoweza kukusababishia umauti.
 
Asante kwa kutujuza haya, tuelimishane na kuhimizana kwenda sipitali kwa uchunguzi zaidi
 
Asante nimeona sababu za kifua kuuma lakini nimefanya cherck up ya Moyo ECG na ECHO nikaambiwa sina tatizo la moyo lakini bado napata maumivu na kichwa kina vurugu nyingi sana kama sio mimi yaani siwezi kupanga ratiba ya mambo yangu kabisa naomba ushauri wako namba 0754418184
 
mzee umepona?
 
Mkuu hicho kipimo cha ECHO ni Tsh ngapi?

Nataka nijue maana nataka nikapime!
 
Asante nimeona sababu za kifua kuuma lakini nimefanya cherck up ya Moyo ECG na ECHO nikaambiwa sina tatizo la moyo lakini bado napata maumivu na kichwa kina vurugu nyingi sana kama sio mimi yaani siwezi kupanga ratiba ya mambo yangu kabisa naomba ushauri wako namba 0754418184
Pole sana
 
Back
Top Bottom