HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO
Kumb.Na A30/MMC-237/vOL. II/19 Trehe:19 machi,2012
Makatibu wa Vyama vya Siasa (W)
Manispaa ya Morogoro
YAH: KUZUIA KUJENGA OFISI ZA VYAMA KATIKA MAENEO YA MASOKO,VIUNGA VYA BUSTANI ZA HALMASHAURI YA MANISPAA NA MAENEO MENGINE YANAYOMILIKIWA NA MANISPAA YA MOROGORO.
Naomba urejee kichwa cha habari hapo juu.
Kumezuka mtindo wa baadhi ya Vyama vya Siasa kupeperusha bendera au kujenga mawe ya msingi ya vyama katika maeneo yanayomilikiwa na Manispaa.napenda kuwafahamisha kuwa ni marufuku kwa chama chichote cha siasa kujenga jiwe la msingi la chama au kuweka bendera katika maeneo yote yanayomilikiwa na Manispaa yakiwemo masoko,viunga vya bustani au stendi za mabasi nk.
Hii ni kwasababau maeneo haya ni ya watu wote wakiwemo wanachama wa vyama vya siasa na wasio wanachama wa vyama hivyo.
hivyo kwa wale ambao wameweka bendear za vyama vyao katika maeneo hao nawaomba kuziondoa harka kabla ya tarehe 23/03/2012 vinginevyo Manispaa italzimika kuziondoa.Naomba hili lizingatiwe ili kusije kukatokea kutokuelewana kusiko kwa lazima.
Nawatakia kazi njema.
J.A . SIMBEYE
MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO
NAKALA: Mkuu wa Wilaya
Morogoro
Mkuu wa Wilaya,
Morogoro
Watendaji wa kata wote,
Manispaa ya Morogoro - hakikisheni agizo hili linatekelezwa
Afisa Masoko
Manispaa ya Morogoro - Watangazieni wahusika
Wakuu nawakilishaa,nafuatilia majibu ya Katibu wangu wa wilaya na nitayaweka humu jamvini soon!