Marekani wanakwama wapi?

tatizo ni magavana wa chama pinzani hawataki kuweka ffu yao mtaani, wao wamekazana kuyaita maandamano ni ya haki na wanafanya maksudi wakidhani kwamba wananchi watamchukia trump ila kibao kimewageukia wengi wamelazimika kutekeleza kuwaweka ffu japo sio kama inavyotakiwa na ndio maana maandamano hayaishi kwasababu upinzani wanataka yasiishe.

amani ni kitu muhimu kwa sasa trump kaona magavana wana kiburi hivyo atatumia madaraka yake kuliweka jeshi mtaani waende sawa na hao wahuni wanaoshabikia kifo cha mwenzao kwa kutumia mwanya wa maandamano kuibia watu majumbani na madukani mwao.
 
Maandamano yamekuwa yakiendelea ila vurugu zimepungua sana si kama hapo awali. Maandamano yamekuwa ni ya amani zaidi kwa sasa. Hilo ni jambo zuri.

Pia, sheria imeanza kuchukua mkondo wake. Wahalifu wamekwisha funguliwa mashitaka huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kuhakikisha haki juu ya kifo cha George Floyd inapatikana.
 
Unasifia demokrasia kwenye hayo maandamano hali ya kuwa hayo maandamano yanatokana na vifo vya watu weusi kuuliwa na polisi na haki haitendeki.
... sijui unataka haki gani itendeke wakati tayari wahusika ndani ya muda mfupi wameachishwa kazi na kufunguliwa kesi? Wananchi wameachwa wa-practice haki yao ya kikatiba ya kuandamana kuonesha hisia zao.

Unamkumbuka Michael Kamuhanda yule RPC wa Iringa aliyeamuru Mwangosi apigwe bomu? Unamkumbuka yule askari aliyelipua bomu? Ni miaka mingapi imepita? Wako wapi? Hata kama una chuki binafsi na Marekani penye ukweli kubali tu Mkuu.
 
Kwani hilo ndio tukio la kwanza kwa Polisi mzungu kuuwa mtu mweusi huko US? Ndio maana nasema hayo maandamano ni kuonesha kuchoshwa kwa hayo mauji ya watu weusi pamoja na ubaguzi kwa muda mrefu.

Haya mauji yapo sana tu huko US.
 
Kwani hilo ndio tukio la kwanza kwa Polisi mzungu kuuwa mtu mweusi huko US? Ndio maana nasema hayo maandamano ni kuonesha kuchoshwa kwa hayo mauji ya watu weusi pamoja na ubaguzi kwa muda mrefu.

Haya mauji yapo sana tu huko US.
... na ni weusi tu ndio wanauwawa na polisi huko US?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…