Kuna vitu vingi kuangalia kwenye mapenzi lakini nakupa hivi vitatu tu kwa leo:-
1) Mawasiliano= ukiwa huna mawasiliano na mpz wako ujuwe huwezi kudumu nae. wanawake au wanaume wengi huhitaji mwenza mwenye kuweza kumsaidia kimawazo pia kuongelea future yao na changamoto za maisha yao ikiwa mmoja wao msiri,sio muongeaji ujuwe kutakuwa na maslahi kwa mmoja na yakisha utasikia wameachana.
2)Uvumilivu= ikiwa mmoja wenu ana hasira sana au sio mtu mwenye kuchukuwa stahmala kwenye mapenzi basi hakuna kudumu kwenye hilo penzi kwasababu binaadamu tuna uwezo tafauti wa hisia na kiakili pia unaweza kumuona anakujali ila uvumilivu hana kabisa ila kama atatumia wakati wa kufahamishana basi pendo lenu linaweza kudumu kwa mfano mwalimu wa shule ana wanafunzi hodari,wa hafadhali na kichwa ngumu. endapo hatoweza kuwa mvumilivu kwa hafadhali na kichwa ngumu basi milele hawatafaulu ndio sawa na mpz au mkeo.
3) Pesa= Pesa sio mapenzi ila kwa machoni inavutia sana na moyoni pia,Leo unataka kujifanya unakwenda na wakati huku ukijua huna kitega uchumi chochote kwenye maisha au utakuta anasa mbele kuliko future ya maisha yako mfano Elimu huna,chanzo cha mapato huna lakini unataka uwe kama Wema au Diamonds kimaisha umesahau kama Diamonds alikuwa akiuza mitumba na kapita changamoto nyingi tu mpaka akafanikiwa kimaisha. kwahio utakuta mapenzi mengi huisha ukiwa huna hela nayo pia ukimuona mwanamke au mme anakuomba sana hela ujuwe sio wewe tu anaekuomba hio hela ila wapo na wengine ndio vitega uchumi vyake.