Mapenzi ya dhati yanajengeka na mazoea

saudari

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
2,655
Reaction score
2,783
Leo nataka tujadili na kuulizana kuhusu suala hili, maana nimekuwa niiskia watu wengi wanaliongelea kwa mitazamo tofauti, kwenu nyie mliokuwa katika ndoa na mahusiano ya muda mrefu, mnaonaje dhana hii ya mapenzi ya dhati na mazoea.

MTAZAMO WANGU.
Binafsi, napenda niseme haya:- Miongoni mwa mapenzi ya dhati na matamu hujengwa na mazoea baina ya wapendanao, Mke na Mume wanapozoeana na Kufahamiana, kunakuwa na Uhuru baina ya Wapendanao hawa, Uhuru huu ukitumiwa vizuri kwa kuzingatia Heshima na Mipaka, wanandoa hawa wanakuwa kama ndugu, kitu kimoja au mwili mmoja.

Na ndio maana ikitokea wanandoa wamepata bahati ya kuona bila kufahamiana au kujuana, mwanzoni kunakuwa na maisha ya ukimya na uoga hasa kwa mwanamke, lakini kadri anavyozidi kuishi na mumewe, humzoea na kumpenda zaidi.
Pia kimaumbile, mapenzi ya mwanamke huja na kuongezeka baada ya kumzoea na kuishi muda mrefu na Mumewe au Mpenziwe.

Kwa kupitia hoja hizo, natetea wale wenzangu na mimi tunaosema kwamba mapenzi ya dhati yanajengeka na mazoea, lakini mazoea hayo yawe yanazingatia heshima na uhuru wenye mipaka.

Nawasilisha.
 
hilo nakubaliana nalo 100% kulingana na uzoefu nilionao
 
Hayo usemayo ni ya kweli,ila sema tu kuna baadhi ya mambo ambayo wapenzi huacha kufanyiana mara wanapozoeana.mf pigiana simu ya mara kwa mara,hugs za evry 2 mins na out za mara kwa mara haya mambo mara nyingi hufanyika wapenzi wanapokuwa ndo wametoka kuoana but muda kidogo ukipita baada ya hapo mambo hubadilika eiza kwa ajili ya kupata watoto au kuzoeana sana.
 
Kwa upande wangu nilikuaga nampaga out za kufa mtu, hii hutokana na kujitahidi kumvutia upande wangu ila baada ya kumpata, out inakuwa mara moja moja lets say j'pili kwa j'pili.
Hii ni kwasababu tumeshazoeana japo inaleta raha ya peke yake pale unapotokanae.
 
ni kweli kabisa,ila hapo mwisho ni uhuru usio na mipaka
sio upo huru na mtu while simu yake huruhusiwi kushika,password za mail fb ,benk hujui ,ni uhuru gani huo sasa? uhuru mzuri ni kujiachia full full kila kitu kiwe exposed!
 
mamito utapewa password zitafunguliwa nyingine 10 huzijui......furahia uhuru mtakaopeana usichoshe kichwa kufikiria mengine......binadamu mwache kama alivyo
 
mamito utapewa password zitafunguliwa nyingine 10 huzijui......furahia uhuru mtakaopeana usichoshe kichwa kufikiria mengine......binadamu mwache kama alivyo
ahahaaa annanza kiushi kiinvisible
 
mamito utapewa password zitafunguliwa nyingine 10 huzijui......furahia uhuru mtakaopeana usichoshe kichwa kufikiria mengine......binadamu mwache kama alivyo

Muda mwingine utajikuta unajitafutia matatizo mwenye, chamsingi ni kuaminiana ila kwenye walakini si vibaya kuchunguza kwa kina na sio kukurupuka.
 
Heshima, upendo na uhuru wenye mipaka.

Naona ndio msingi mkubwa katika mahusiano!
 
nakubaliana na ww mkuu ili lzma kila mmoja amzoee mwenzake na kumjua vzr, mahusiano yoyote ambayo kila 1 hamjui mwenzake kiundan,na hajamzoea hua magumu sana na mara nyingi hayadumu
 
saudari
Naunga mkono hoja maana mambo mazuri hayataki haraka.
 
Last edited by a moderator:
Kweli saudari Pendo lianzalo taratibu huisha taratibu na lile la haraka huisha haraka.
Mizizi ya penzi la taratibu huenda mbali sana na hufungua mengi.
 
Last edited by a moderator:
nakubaliana na ww mkuu ili lzma kila mmoja amzoee mwenzake na kumjua vzr, mahusiano yoyote ambayo kila 1 hamjui mwenzake kiundan,na hajamzoea hua magumu sana na mara nyingi hayadumu

You got my point.
 
Licha tu ya kuzoeana majukumu pia huongezeka mara mnapofunga ndoa,mwanaume kutafutia familia riziki na mwanamke kutaunza nyumba,mtapata saa ngapi muda wa kufuatana kama kumbi kumbi na out za mara kwa mara?
 
Ndo maana mimi nafanyaga j'pili kwa j'pili japo sio saaana ila inasaidia hata kupunguza stress.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…