Mapenzi kama jalala

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
Mapenzi Jalala

1 Mapenzi kitu ajabu, kumbe anaye mwingine
Waliya bila sababu,yeye yupo kwa Zidane
Hata bila ya sababu , ataenda kwa Zahabu
Mapenzi kama jalala, utupapo waokota

2 Ya kama Mondi na Zuchu, kila mtu ana lake
Moyo ungali na uchu, kupata kilicho chake
Kuna wakati mkuchu, kusonona ndani mwake
Mapenzi kama jalala, utupapo waokota

3 Utayempenda kweli , ila atakukataa
Ataangalia mali, hata yakiwa makaa
Hiyo ndio ahwali, sasa katika dunia
Mapenzi kama jalala, utupapo waokota

4 Utamuwaza yeye tu , asitoke akilini
Naye moyoni ni Patu, amuhitajie ndani
Kwa sasa kama upatu, leo weye kesho Dani
Mapenzi kama jalala, utupapo waokota

Abuuabdillah ✍️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…