matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,511
SafiSio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.
Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasabaratike na kudharirika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.
Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.
Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yakiyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.
Kabla hujakurupuka na kukurupushwa na imani mwendokasi za kibishoo za kisasa za kukamia watu na kuwatakia mabaya, Mwambie Mungu akufunulie aina ya ya vita unavyopigana ili ujue mahali sahihi pa kuelekeza mashambulizi yako kwa ufanisi.
Luka 9:54 ~56
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Ni hayo tu.
Karibu kwa neno lolote. Kama umeelewa andika amina.
Usimsikilize Malisa. Msikilize Yesu.Clear Malisa anasema adui yako muombee mabaya
Mathayo 5:43-44,46-47Clear Malisa anasema adui yako muombee mabaya
Watu wengi wanafunga na kuomba wakiongozwa na roho za korosho, visasi, jazba, chuki na kukamia watesi wao.Hata miujiza inatakiwa kufanywa bila kumdhuru mwingine, Wazungu wanasema Don't direct negative energy to other person.
Leo umeongea Kitu kizuri Sana matunduizi ni kitu kila siku nakipigania "Upendo"..Hujui tuUsimsikilize Malisa. Msikilize Yesu.
Tatizo waumini wa kisasa mnapenda watu kuliko kauli za Mungu.
KabisaLeo umeongea Kitu kizuri Sana matunduizi ni kitu kila siku nakipigania "Upendo"..Hujui tu
Ukikosa Upendo hata unacho Sali,Imani yako ni bure...
1 Wakorintho 13:13
[13]Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
hapa nimekuelewa Mkuu,[emoji2936][emoji2935]Sio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.
Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasabaratike na kudharirika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.
Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.
Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yakiyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.
Kabla hujakurupuka na kukurupushwa na imani mwendokasi za kibishoo za kisasa za kukamia watu na kuwatakia mabaya, Mwambie Mungu akufunulie aina ya ya vita unavyopigana ili ujue mahali sahihi pa kuelekeza mashambulizi yako kwa ufanisi.
Luka 9:54 ~56
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Ni hayo tu.
Karibu kwa neno lolote. Kama umeelewa andika amina.
Malisa ndio TAKATAKA gani?Clear Malisa anasema adui yako muombee mabaya
Takataka ni nini?Malisa ndio TAKATAKA gani?
Je, mnao waamini ya kuwa taifa teule la wana wa Mungu israeli wanawapenda adui zao!? (Wapalestina)Mathayo 5:43-44,46-47
[43]Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
[44]lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
[46]Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
[47]Tena mkiwasalimia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Asilimia 30 za wa le wayahudi hawamuamini Yesu, 70 iliyibaki hawaamini Mungu yoyote.Je, mnao waamini ya kuwa taifa teule la wana wa Mungu israeli wanawapenda adui zao!? (Wapalestina)
Mkuu Sijawahi Kuwa upande wa Kidini wowote wala sijawahi kuwa Katika upande wowote wa Waabuduo mabaya..Je, mnao waamini ya kuwa taifa teule la wana wa Mungu israeli wanawapenda adui zao!? (Wapalestina)
Shetani apite mbaliii asee