Manqoba Mngqithi ni kocha mzuri

kibaigwa finest

Senior Member
Joined
Oct 18, 2026
Posts
189
Reaction score
208
Yanga SC hawako sawa, kuna sehemu ina shida binafsi sidhani shida ni Kocha wao. Nimejiuliza kama wachezaji wanapata nafasi namna hii na hawafungi Kocha unataka afanyaje?

Leo walikuwa na uwezo wa kuweka rekodi ya kushinda mabao mengi ugenini hatakama ugenini kwenyewe ingekuwa Madagascar ya Chamazi, lakini msingi ni nini kipo nyuma ya hiki kinachoonekana kwa wachezaji wa Yanga? Hapo Shalulie alishakosa na yeye kwenye hicho kipindi cha kwanza, fikiria mapochi hayo unasema Kocha ana shida.

Timu ingefunga kwenye hizi nafasi wangeenda halftime walau na bao 3, lakini walienda na 0-1. Viongozi wanaapaswa kufanya kazi yao sio kuacha tu watu wanatafuta sababu rahisi ya Kocha hana uwezo, lakini benchi la ufundi nalo lifanye tathmini, lichukue hatua.

Group Stage hakujawahi kuwa kwepesi hizi timu kama CFFA mbovu kwa kiasi hiki zinaishia huku huku mara nyingi.

Ruhusuni maoni kutoka nje ya waliowazunguka na chawa hatakama yatakuwa yanakera lakini kama yanawapa kitu cha kukifikiria chukueni fanyieni kazi, kuliko kutaka kusifiwa tu."

AMESEMA MCHAMBUZI WA SOKA, BIN KAZUMARI

Je, NIUPI MTAZAMO WAKO KATIKA HILI ?
 
Nadhani changamoto ni kutokujiamini kwa wachezaji sijui imekuaje. Au kama sio hivyo, basi wameshalogwa na timu pinzani maana wanasifika kwa uchawi
 
Huyu kocha anataka kutupa kombe la Afrika halafu Simba wanatufanyia fitina tumfukuze
 
Nadhani changamoto ni kutokujiamini kwa wachezaji sijui imekuaje. Au kama sio hivyo, basi wameshalogwa na timu pinzani maana wanasifika kwa uchawi

Saivi mpiravi ni uwekezaji ndani na nje ya uwanja hizo Iman za kishirikina hazisaidii chochote
 
Kama huyu anasifia basi kocha hatuna🤣
Kwa uelewa wangu mdogo wa mpira naona shida ipo kwenye baadhi ya wachezaji kutoendana na mfumo wa high pressing, Ngoma, Toure na yule Mcomoro watupishe dirisha dogo, hawaendan na mfumo plus baadhi yao hapo umri umewatupa!
 
Ni kocha mzuri ila apunguze kiburi, dharau na kufokafoka. Moira unahitaji utulivu na maamuzi ya busara.
 
Duombia habari ya mjini
 
Huyu kocha anataka kutupa kombe la Afrika halafu Simba wanatufanyia fitina tumfukuze
Ukiona kocha anasifiwa na wana Simba na kutetewa na wana Simba basi unapaswa kutathmini mambo kwa kina. Rodrick umeamia lini Yanga? Hersi akifanya mchezo mashindano ya ndani anapoteza mataji na ligi ya mabingwa ataishia makundi. Akiendelea na Manqoba Yanga haitopata mafanikio msimu huu. Na pia akimuacha Manqoba, anatakiwa amlete kocha mwenye akili kubwa ya kiufundishaji, anayeweza kufanya vitu viwe sawa kwa muda mfupi. Sijui kama bahati hiyo ataipata tena, baada ya kupoteza bahati hiyo kwa kocha Miloud.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…