MAnispaa ya temeke inatafunwa

Snitch

Senior Member
Joined
Oct 22, 2011
Posts
165
Reaction score
42
WIZI WA FEDHA ZA UMMA MANISPAA YA TEMEKE::
Inasikitisha ktk kipindi hiki ambapo Serikali inasisitiza kuziba mianya ya Wizi na Upotevu wa Pesa Manispaa ya Temeke ndio kwanza Inazidisha Wizi kwa kuunda Mtandao Maalum wa Wezi unaoongozwa na Meya(Abdalah Chaurembo),Mkurugenzi(NASEEB Mbagga) na wakuu wa Idara baadhi ikiwemo Idara ya Maji,Idara ya Afya,Mweka Hazina na Afisa Ugavi.

Wizi hufanyikaje?:Maskini kwanza Madiwani wamenyimwa uwezo wa Kusema kwa kuwa Meya ndio hataki waongee na amegeuka kuwa msemaji wa Wataalamu kutokana na Kunufaika na Wizi wanaofanya.
Mfano:
1)Idara ya Maji iliidhinishiwa pesa zaidi ya milioni 30 ili kusafisha visima vya Maji lkn zikaishia Kusafisha Matumbo ya Wezi hao bila Huruma.

2.Mganga Mkuu aliyehamishwa GWAMAKA MWABULAMBO alishirikiana na Mtandao huo kuchota fedha za mafunzo ya mawasiliano kwa watumishi wa idara afya lkn fedha zilizotumika ni milioni 8 kuliko milioni 26 na mwezi mmoja tena BAADA zikaidhinishwa milioni 20 kwa mafunzo hayo hayo maskini Temeke.....

3. UKABILA ndio umekua Sera kuu;Kwa sasa sisi ambao hatuna historia ya Kupewa Tenda ndani ya wilaya hadi uwe aidha Mpare au Mchaga tizama kazi za ujenzi wa majengo na miradi ya barabara ili ujue angali ukabila wa Mkurugenzi na Mweka Hazina,Idara ya Maji na wanaopewa Tenda mbalimbali,,,nasikia hata wakuu wa Idara wasio na historia ya kaskazini wanadhalilika kweli na ambao wanapeta ni wale ambao waliletwa na mkurugenzi Kama afisa Ugavi CHACHA ambaye ametoka Biharamulo alikotoka mkurugenzi ambaye amemleta kuweka mtandao WA WIZI vizuri

Madiwani Tumetengwa Wanaonufaika ni wachache ambao wako kamati ya mipango miji ambao mara kadhaa wamekuwa wakipata mgao toka kwa Meya mfano ni Mwekezaji wa petrol station inayotarajiwa kujengwa eneo la quality center INDUSTRIAL TECHNICAL SERVICES LTD Kiwanja no 1BE.P kitalu no LOT 20 chang'ombe matumizi ya kiwanja ni viwanda namba ya maombi ya Kibali ni T354/2017 kilichoombwa tarehe 30/11/2017 ambapo wenzetu wakipata Mgao toka kwa Meya sasa tusiopata tunahangaika tunatamani kugawana fito maana Meya anatunyima migao ya kutosha na Anatetea kwa kuwa ni mnufaika, kwa sasa Anatembelea gari alilopewa na mkurugenzi analitumia vibaya kwa kusafiri nalo hadi Lindi shambani kwake Duuh Halmashauri imekufa....

Hivi Leo tarehe 09/03/2018 amepewa gari la halmashauri namba SM 10073 na mafuta karibuni lita Mia mbili hadi nyingine zimejazwa kwenye madungu kupeleka mabati NG'APA Lindi akisingizia ni ya mkubwa serikalini sijui ni nani?

Amekuwa akitumia jina la waziri mkuu vibaya na kuwatishia watendaji na kusema yeye anaushawishi jambo ambalo Limewavunja moyo.

MKURUGENZI NASEEB MBAGA huyu amekuwa ni tishio amekuwa akijitutumua kuwa yeye ni afisa usalama na kwamba Ikulu anavijana wake akisema hata mpambe wa Rais ni kijana wake lakini pia yeye ni rafiki na katibu mkuu tamisemi na kwamba mabadiliko yote ya wakuu wa idara ni kutokana na kumweka mkononi MUSA IYOMBE jambo ambalo miongoni mwetu tumeanza kuliamini.

Haya niliyoyasema naomba mamlaka za uchunguzi wafike watashuhudia yote kabla funika kombe haijaanza.

Tunajiuliza kwa haya yote Vyombo vya Ulinzi na Usalama mbona vimelala!Wako wapi Usalama wa Taifa au wanamlinda mwenzao ?au Kazi ya usalama ni kuilinda CCM tu?wako wapi TAKUKURU au kazi yao ni kuhoji tu waliokula pesa za TEFA??wako wapi POLISI au kazi yao ni kuzuia mazishi ya Tambwe hiza tu?Tafadhali Zindukeni Mumsaidie Mheshimiwa Rais Kupambana na Mtandao huu wa Wezi.

Bado part 2.

Ndimi mwana Mtoni
 
Dili za waafrica....akinyimwa mmoja tu ujue linabumburuka haraka.

Lakini...kn ukweli sehemu ngoja walinzi waje kuchunguza...
 
Watu wengine mna bore sana. Unajiita diwani halafu na wewe unataka mgawo? Kama ni diwani si kuna vikao vya madiwani kwenye Baraza la Halmashauri ni lini umewahi kuwasilisha hoja kuhusiana na haya?
 
Manshindwa kumpiga juju tu maana kwa nguvu hizi za kawaida watakuziba mdomo sasa hivi
 
Wewe mwenyewe unataka mgao, ungepewa usingesema sio? wewe mwenyewe ni mtuhumiwa unatakiwa uchunguzwe! duuuu! Usilete kashifa kwa watu ambao innocent na sababu zako za kisiasa, baba hakuna mseleleko siku hizi, hata hao unaowahisi ni siasa zako tu zinakuzingua!
 

Bora jiweke wazi !
Ila achene njaa. Mnaleta mambo pale msiponeemeka ! Wao vs Sisi
 
Yan madiwani mmetengwa wanakula wachache:
1.Ina maana msingetengwa mngeendelea kula kimya kimya na wala usingelalamika.
2.Inaonekana huna pa kwenda kusemea ndo mana umekimbilia jf.
3.We ni diwani wa Chama gani ,kama ni CCM ,inamana huna number za rais umweleze hayo?.
4. Loading.....
 
Rais Magufuli bila shaka kabla ya kulala huwa anameza 'pain killer' maana kuongoza nchi iliyooza kiutendaji na kiuadilifu ni 'kununua' maumivu ya kichwa.Ana kazi ngumu mno kunyoosha mambo.Mh.Rais tuna wasomi teeeeele nchi hii,tatizo la wengi wao ni NAKISI YA UADILIFU.Na haupatikani uadilifu ila kwa MCHA MUNGU.
 
Meya na mkurugenzi hawawezi kufanya lolote bila baraza la madiwani
 
Topic yako haiko vizuri,iko kishabiki sanaa na hii imeondoa maana na lengo lako,maana imeonyesha ni majungu kutoka kwa diwani wa upinzani
 
Mku kwa hiyo rushwa kama kaida ila ni mipango imebadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…