tonge nyama
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 380
- 502
Wakalale tu hawa jamaa manake kazi yao wanaifanya kama waganga wa kienyeji. Majuzi walisema kuna elnino inakuja baadae tukaambiwa mkondo umeihamisha elnino so haitakuwepo. Leo wanatwambia kuna mvua inakuja. Kuna jipya gani kwani nani asiyejua kuwa kwasasa kwamba kuna mvua za vuli? Wameshindwa kazi hao!!!!!
nasikia huko kanda ya ziwa especially Mwanza kunanyesha, pengine walikuwa wakilenga maeneo hayo
Linalohusu mkuu katika hili ni accuracy katika taarifa zao wala siyo suala la hali ya hewa kubadilika badilika. Wait a minute..... sijaona sababu ya kutokwa na povu hapa!!!Mi nafikiri wabongo tuache kuwa wavivu wa kufikiri aka vilaza, ni nani asiyejuwa kuwa hali ya hewa huwa inabadilika kila mara? Ni jukumu la mamlaka hii kutujulisha mabadiliko hayo kila yanapotokea, kubadilika badilika kwa taafifa hizi haimaanishi kwamba mamlaka ni wababaishaji bali ndio hali halisi ya kinachotokea angani kwa muda husika. Katika nchi za wenzetu wanaojua nini maana ya utabiri wa hali ya hewa media zao kama vile BBC na CNN wapo serious kiasi cha kuruhusu kutolewa kwa updates za weather kila baada ya nusu saa na taarifa hizo huwa zinabadilika badilika. Nafikiri hatuna sababu ya kutokuipongeza mamlaka ya hali ya hewa kwa kujitahidi kuwa karibu nasi hata katika mitandao ya kijamii Tanzania Meteorological Agency | Facebook ili kutupa taarifa. Ni jukumu letu kama wanajamii kufuata shauri za kitaalamu na si kubeza.
Linalohusu mkuu katika hili ni accuracy katika taarifa zao wala siyo suala la hali ya hewa kubadilika badilika. Wait a minute..... sijaona sababu ya kutokwa na povu hapa!!!
Hello bandugu!!
Nimepita facebook page ya TMA leo na nimekutana na taarifa ya uwezekano wa ongezeko la mvua katika baadhi ya mikoa katika siku mbili zijazo kuanzia kesho 01/11/2012. Kwa maelezo zaidi gonga Tanzania Meteorological Agency | Facebook