Mambo ya Kuzingatia katika Uchumba

mij

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
1,993
Reaction score
2,128
Kuna mambo mengi hutokea katika kipindi cha uchumba kwa hivyo ni bora tujulisahane. Si kwamba nayafahamu yote ila ninaanzisha mada naomba wanajamii tujadili ili kusaidiana pale mambo yanapokwenda kombo.

SASA NAANZISHA:
1. Uchumba si mkataba wa kudumu, hivyo unaweza kuvunjika muda wowote.

2. Si vema wala busara kudai ( hasa wanaume ) gharama za yale yote uliyoyafanya kwa mchumba wako baada ya uchumba kuvunjika.

3. Msianzishe miradi pamoja kwani bado hamjaingia katika ndoa, wengi wamedhurumiwa baada ya uchumba kuvunjika.

4. Usiingie gharama za kumsomesha mtu ambaye huna uhakika kama mtafunga ndoa na kuishi pamoja. Hapa wanaume wengi yamewakuta na kujuta kuzaliwa. Utakuta mtu kamsomesha mchumba(msichana) mpaka chuo kikuu, then anaachwa kwenye mataa na kuolewa na mwingine.

5. Pawe na uhuru sio kila wakati mpo pamoja. Kumbuka kila mtu anahitaji kuwa peke yake wakati fulani ili aweze
kutakafari mambo.

6. Kuwa makini na maneno yaanyosemwa juu ya mchumba wako, usikurupuke katika kutoa maamuzi usije ukaja
kujuta.

7. Kama ana tabia mbovu ambayo ameshindwa kuiacha mkiwa wachumba unapaswa kuwa makini. Usijidanganye hawezi kubadilika akiingia katika ndoa. Mambo yakakuwa magumu zaidi. Achana naye huyo si wako, Mungu atakupa mwingine.

8. Mambo ya "bila kaka/dada A mimi najinyonga" hayana msingi. Huo ni upungufu wa akili na ujinga uliopitiliza. Yeye ni nani mpaka akufanye upoteze uhai? Akikuacha chukua hamsini zako na maisha lazima yaende.

UNAWEZA KUONGEZA MENGINE.
 
sex sio kipimo cha mapenzi,hapa wadada wamelizwa sana lol,unadhania ukimyima hatokuacha mnh
 
kingine ni 'come and stay' leave kuna watu wanazipinga vita ila naona zinasaidia kumjua mtu kwa kila kitu,hizi ndoa za siku hizi lazima uwe na short starter session na umpendaye muone kama mko compartible lol:rockon::rockon:
 
sex sio kipimo cha mapenzi,hapa wadada wamelizwa sana lol,unadhania ukimyima hatokuacha mnh

na wataendelea kulizwa.....man has dominated woman to her injury always has been always will be
 
Jestina uko deep...!

wangekua wanayasikia haya...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…