Leo padri wenu Mtarajiwa napenda kuwapa kwa kifupi kabisa MALENGO YA KUINGIA KATIKA TAASISI YA NDOA
1. Kwa manufaa ya wanandoa wenyewe. Kumbukeni mnapoingia katika mahusiano ni kwa madhumuni ya kuungana kimwili na kiroho mkiishi kwa upendo na uaminifu kati yenu wawili. Kwa kiapo chenu cha ndoa kila mmoja anajitoa kikamilifu na kiaminifu kwa mwenzake kumpenda na kumheshimu siku zote za maisha yake. Kwa kiapo hicho mnaapa kuishi pamoja kufuatana na mpango wa mungu muumba wenu. Kwa kiapo chenu mbele ya kasisi aliye shuhuda wa kanisa juu ya hicho mnachoapa mnajifunga kuwa waaminifu mbele ya mungu na mbele ya umma.
2. Kuendeleza shughuli ya uumbaji kwa kuwapokea kwa furaha watoto mtakaojaliwa na mungu, kuwatunza, kuwapenda kwa kuwapa magtaji yao yote ya kiroho na kimwili bila kusahau ya kimaadili. ITAENDELEA