Rubawa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2015
- 2,055
- 3,267
NA MOHAMMED ABDULRAHMAN
Mapema mwezi huu wa Februari mahakama ya katiba nchini Malawi ilitoa uamuzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na kumaliza mvutano uliosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa Rais mwezi Mei mwaka uliopita, ambapo Rais Peter Mutharika alitangazwa mshindi. Iliamuru uchaguzi huo urudiwe katika muda wa siku 150. Bila ya kuchelewa Mutharika akaupinga na kukata rufaa akisaidiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo nayo pia ikakata rufaa ikisisitiza matokeo yaliokuwa sahihi, hayakuwa na utata wowote. Jumatano wiki iliopita iliopita, rufaa zote mbili zikatupiliwa mbali.
Mutharika alikuwa ametangazwa mshindi kwa asilimia 38.5 ya kura dhidi ya mpinzani wake, kiongozi wa chama cha upinzani Lazarus Chakwera aliyepata asilimia 35.41 ya kura na makamu wa zamani wa rais Saulos Chilima asilimia 20. Kilichofuata baada ya matokeo kutangazwa kilikuwa ni maandamano dhidi ya serikali, wafuasi wa upinzani wakihoji uhalali wa matokeo na kupinga hesabu
zilitotangazwa na tume. Wakiungwa mkono na viongozi wao, walidai kulikuwa na ushahidi wa mizengwe na wizi mkubwa wa kura.
Mutharika alikwisha apishwa baada ya tume kushikilia kwamba matokeo yalikuwa sahihi na hakukuwa na dosari zozote kubwa ambazo zingeweza kubadili matoke . Uamuzi wa mahakama ulifuatia kesi iliofunguliwa na upinzani kupinga matokeo ambapo wanasheria wao waliwasilisha vielelezo na ushahidi uliokubaliwa na majaji kwamba kweli kulikuweko na kasoro kubwa, ikiwemo rushwa. Baada ya miezi sita ya kuisikiliza kesi hiyo hatimaye jopo la majaji watano waliobobea likatoa hukumu kwamba uchaguzi urudiwa na kusisitiza kuwa Wamalawi wana haki ya kuwa na uchaguzi huru bila mizengwe na kulitaka bunge lizingatie kuitaka tume ya uchaguzi iitishe uchaguzi mpya mnamo muda wa siku 150.
Kwanza hukumu yake ya awali dhidi ya matokeo ilikuwa sawa na kutumia ujumbe kwamba hakuna aliye juu ya sheria na chombo kinachopewa dhamana ya kuandaa zoezi kama hilo kinapaswa kuwa kisichoelemea upande wowote na kwamba ili demokrasia iweze kushamiri ni lazima taasisi zinazoisimamia ziwajibike na kulindwa kisheria. Wakati uamuzi wa mahakama ukiwa pigo kubwa, kabla ya Mutharika mwenye umri wa miaka 79 kukata rufaa alilihutubia taifa. Katika hotuba hiyo ya dakika tatu na sekunde 55 alisema, ”Kitu muhimu zaidi ni lazima tuilinde katiba yetu na kuhakikisha Malawi inabakia imara na yenye utulivu. Akaongeza ,Kama walivyo Wamalawi wengi timu yangu ya wanasheria na mimi mwenyewe tuna shaka shaka kubwa na uamuzi wa mahakama ya katiba. Tunaizingatia hukumu hii kuwa ni ukiukaji mkubwa na jaribio la kuhujumu matakwa ya umma. “ Mutharika akasema watakata rufaa kupinga hukumu iliotolewa. Akafanya hivyo.
Jumatano iliopita Mahakama ya rufaa ikatoa huku yake na kuipinga rufaa ya Mutharika na ile ya Tume ya uchaguzi. Kilichoamuliwa na mahakama mjini Lilongwe kuanzia kuamuru uchaguzi wa Rais urudiwe hadi kutupiliwa mbali rufaa zote mbili ya Rais Mutharika na Tume ya uchaguzi , ni ushindi sio tu kwa demokrasia bali heshima kwa mahakama iliojitenga na ushawishi wa kisasa ili kutenda haki ikiliweka taifa kwanza .Malawi ni nchi ya pili barani Afrika ambako matokeo ya uchaguzi wa rais yamepingwa kisheria. Ya kwanza ilikuwa Kenya 2007, upinzani ulipopinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya mgombea wao Raila Odinga.
Kenyatta alishinda uchaguzi wa marudio kama ilivyoamriwa na mahakama, baada ya Odinga kuususia kutokana na kutorekebishwa kwa tume ya uchaguzi kama wapinzani walivyodai. Ni mfano wa kuigwa kwa nchi nyingi ambako mahakama bado ni kikwazo katika kutenda haki panapohusika na chaguzi , mara nyingi zikionekana kudhibitiwa na watawala kama ilivyo na tume za uchaguzi. Katika baadhi ya nchi neno “ Tume Huru Ya Uchaguzi,” ni katika maandishi tu na sio utendaji, zikiwa mzizi wa dosari zinazoonekana wakati wa uchaguzi.
Mapungufu mengine ni kukaa kimya au kushindwa kuzikosoa nchi zinazokandamiza demokrasia kwa Jumuiya za Kikanda ikiwa pamoja na Umoja wa Afrika chombo kikuu barani humo. Kuhusiana na Malawi hata hivyo, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ilitoa taarifa kuipongeza Mahakama kwa kile ilichosema” Kuilinda Katiba,” ikiahidi kuisaidia katika kukamilisha mchakato huo wa uchaguzi .
Itakumbukwa mara nyingi SADC imelaumiwa kwa kuwa jukwaa la kulindana na mfano mmoja ni katika hali ya kisiasa nchini Zimbabwe wakati wa utawala wa Rais wa zamani Robert Mugabe. Baada ya matokeo ya uchaguzi mwaka 2000 ambapo chama cha upinzani Movement for Democratic Change-MDC kilikishinda chama tawala ZANU-PF, ni aliyekuwa Rais wa Botswana Ian Khama pekee aliyesimama kidete kumkosoa wazi Mugabe kwa kutumia nguvu kuwanyima ushindi wapinzani wake.
Kiu cha Mutharika mwenye umri wa miaka 79 na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje , kutaka kuitawala Malawi, kilianza wakati alipotaka kumrithi Kaka yake Bingu wa Mutharika aliyefariki 2012. Alituhumiwa kuhusika katika njama ya kumzuwia Makamu wa Rais wakati huo Joyce Banda kuchukua wadhifa huo kwa mujibu wa katiba.Katika uchaguzi wa 2014 Mutharika akasimama dhidi ya bibi Banda na kumshinda.
Safari ya Malawi kuelekea demokrasia ilianza 1992, raia waliposhoshwa na utawala wa kidikteta wa rais wa kwanza Dr Hastings Kamuzu Banda maarufu “ Ngwazi,” aliyekamata hatamu tangu uhuru kutoka kwa Uingereza 1964 na mwaka 1971 kujitangaza rais wa maisha. Mnamo mwaka huo alilazimika kurejesha mfumo wa vyama vingi kufuatia machafuko ya umma kupinga ukandamizaji, kupigwa marufuku siasa za upinzani, kukamatwa wanasiasa waliothubutu kumkosoa rais huyo, mauaji na kupotea watu hovyo. Wanasiasa kadhaa walikimbilia uhamishoni, miongoni mwao waziri wake wa mambo ya nchi za nje na mmoja wa waliopigania uhuru Kanyama Chiume. Chiume aliishi nchini Tanzania. Banda alikuwa na mtazamo wa kibwanyenye na wakati alionekana mmoja wa viongozi shupavu kabla ya uhuru, aligeuka na kuwa kiongozi wa kwanza wa kiafrika aliyekuwa na uhusiano na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.
Ulipoitishwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1994 baada ya utawala wa miaka 30 wa chini wa chama kimoja Malawi Congress, Banda alishindwa na Alhaji Bakili Muluzi wa chama cha United Democratic Front, tukio la kihistoria katika kanda ya kusini mwa Afrika. Kiongozi huyo amoja na hayo alistahiki pongezi kwa kukubali kushindwa, akimpongeza Muluzi na kuahidi kumuunga mkono kikamilifu. Ilikuwa hotuba ya kusisimua kutoka kwa mtu ambaye akitajwa kuwa dikteta aliyetawala muda mrefu barani Afrika tena kwa mkono wa chuma. Banda alifariki dunia 1997 akiwa na umr wa miaka 99.
Mbali na umri mkubwa na afya yake kuwa mbaya, inawezekana Ngwazi alipata somo la kujifunza kwa Rais wa nchi jirani ya Zambia Keneth Kaunda (KK) aliyekuwa rais wa kwanza kuheshimu matakwa ya umma dhidi yake katika uchaguzi wa vyama vingi baada ya kufuta mfumo wa chama kimoja. Kaunda alishindwa 1991 na mgombea wa upinzani na mkuu wa zamani wa chama cha wafanyakazi Frederick Chiluba.
Ingawa kisheria Rais Mutharika alikuwa na muda wa wiki sita kukata rufaa na ni haki yake ya kikatiba, lakini tamko lake kwamba atakata rufaa kupinga uamuzi kuitishwa uchaguzi upya, limewashtuwa Wamalawi wengi kwa kuwa Mutharika ni kiongozi msomi, mwanasheria aliyehitimu sheria katika chuo kikuu cha Yale Marekani na kile cha mjini London Uingereza. Wanashangaa kuwa aliipinga hukumu ya mahakama ya katiba , chombo kikuu cha kusimamia sheria nchini humo.
Wadadisi wana wasiwasi kwamba hivi sasa hatua yoyote kujaribu kuzuwia utekelezaji wa uamuzi wa mahakama inaweza kusababisha maandamano mapya ya upinzani. Spika wa bunge Catherine Gotani amesema wao kama bunge watauheshimu. Hapana shaka wamalawi watakuwa wakifuatilia kwa karibu utendaji wa Tume, kuona ikiwa safari hii itatenda haki.
Demokrasia ni mchakato na Malawi ina kila sababu ya kujivunia mafanikio yake katika kuilinda demokrasia na utawala wa sheria ,hasa unapozingatia misukosuko ya kisiasa ni sehemu ya
utekelezaji wa mchakato huo ambapo suluhisho muwafaka huwa ni kupitia kupitia utaratibu wa kisheria ukisimamiwa na mahakama.
Mataifa kadhaa yamefungika, ama kwa mahakama kuingiliwa kisiasa au kuendelea kuwepo kwa katiba zilizopitwa na wakati . Baadhi ya watawala wanapendelea kuziba "viraka" kufanya marekebisho ambayo mara nyingi ni ya kuwafaidisha wao binafsi na vyama vyao, na sio kuandikwa katiba mpya. Sambamba na hayo ukosefu wa kuwa na huru za Tume za uchaguzi ni utata mkubwa.
Chanzo: Raia Mwema / Barupepe: mamohamed55@hotmail.com
Twitter: mamkufunzi
Sent using Jamii Forums mobile app