Nakushukuru sana kwa ushauri wako na yote haya nitayafanyia kazi ASP!!Nenda kwenye duka la wahindi la madawa, labda sijui upo mkoa gani... Maana yana majina tofauti! Mwambie akupe ZANDU ya malaria sugu kwa ajili ya mtoto! Pia wakati unatumia zandu anza kumpa mlonge atlest mbegu mbili daily! Pia kama una kauwezo mpatie juice za nutrients za forever living Alovera Gely na ile development ya kuchanganyia kupunguza uchungu, Kama vp ni pm nikuunganishe na mtaalamu Wa dozi za forever living.
Mimi nipo Kishapu - Shinyanga.Nenda kwenye duka la wahindi la madawa, labda sijui upo mkoa gani... Maana yana majina tofauti! Mwambie akupe ZANDU ya malaria sugu kwa ajili ya mtoto! Pia wakati unatumia zandu anza kumpa mlonge atlest mbegu mbili daily! Pia kama una kauwezo mpatie juice za nutrients za forever living Alovera Gely na ile development ya kuchanganyia kupunguza uchungu, Kama vp ni pm nikuunganishe na mtaalamu Wa dozi za forever living.
Ahsante sana Zemarcopolo kwa ushauri wako.Nishampeleka kwa madaktari kama wa3 ivi ila wote si specialists wa watoto kutokana na mazingira nilipo yaani shinyanga vijijini. Ktk hao,wa1 ndo hakuona kitu kabisaa wakati wa 2 ndo akagundua hiyo malaria5. Wa3 ndo kagundua hiyo malaria 3,2 na 1. Kuhusu namna wanavyopima sielewi,maana utakuta dokta anachukua damu ktk kidole na baadae anakuletea majibu. Sure at the time being,itabidi tucheki na magonjwa mengine kama vile UTI na kupata ushauri zaidi kwa doktari anayempima mtoto. Thanks indeed kwa ushauri wako wa kitaabibu!Pole sana wende. Kwa mtoto wa mwaka na miezi miwili kushindwa kutembea mwenyewe sio tatizo. Kila mtoto huwa anaatiba yake ya kuweza kutembea, kuongea etc. Hivyo swala la mtoto wako kutokuanza kutembea mapema kama ulivyotarajia lisiwe lenye kukupa shaka. Kuhusu malaria. Kwanza naomba kujua huyo mtoto huwa unampima katika kituo hicho hicho kimoja? Je, huwa wanatumia njia gani kumpima? Ushauri wangu ni huu: mpeleke mtoto kupima katika vituo viwili au vitatu tofauti kwa njia ya microscope na njia ya RDT (Rapid diagnostic test). Angalia kama majibu yote yanaonyesha ni malaria na kama kiwango chake kinafanana. Mtoto kuwa na vidudu vya malaria haimaanishi kuwa homa au dalili nyingine alizo nazo zinakuwa lazima zimesababishwa na uwepo wa hivyo vidudu. Kwa mfano mtoto anaweza kuwa na malaria na UTI au ugonjwa mwingine kwa pamoja. Katika hali kama hiyo, iwapo utanendelea kutibia malaria tu, ugonjwa mwingine unapata fursa ya kuwa sugu. Kwa hiyo, kwa mtoto wako kuna haja ya kutafuta sababu nyingine zinazoweza kuwa zimesababisha kuumwa kwake. Pata ushauri wa daktari ambaye atampima mtoto.
Thanks George. Noted!kwa mtoto mdogo wa miaka 1.2 kutumia dawa kali kama hizo (quinine) na kwa kipindi kirefu hiyo pia ni Tatizo. Tatizo sasa siyo malaria bali ni sumu ya hizo dawa. Hospital ya mkoa au Bugando wanaweza kukusaidia kikamilifu kuliko zahanati au hawa jamaa wa pharmacy. Meanwhile mpe fresh orange juice (kamua mwenyewe na dilute by water 1:1)na maji masafi kwa wingi.