Makamba Named 2013 Young Global Leader

Wakuu,
Mr Kafulila, D. Alitoa mchanganuo namna ambavyo sekta ya mawasiliano ingeweza kukusanya kodi ki-halisia kabisa kwa kila simu inayopigwa kwa siku na kwa jumla ya watumiaji woote wa simu za mkononi wangeweza kukusanya zaidi ya Trillioni 13 kwa mwaka.
Laiti yale mahesabu ( sijui nimeyaweka wapi ? ) Yangekuwa yameletwa jamvini na Mr Makamba na kuyafuatilia hatua kwa hatua na kukusanya kwa kiasi hicho cha fedha kama kodi ( kwa sekta ile tu ) hata wangemuita na kumpatia hadhi gani Duniani wala nisingejali !

Ila kwa hilo la kuanzisha tuition camps kwa wanafunzi wa kidato cha nne jimboni kwake ndio la kumpia tuzo ni upuuzi tu

Labda kama huyo demu mshauri wa uchumi alikuwa manzi yake na inawezekana !
 

Hii habari inatikia kichefuchefu. Huyu mvivu wa grade A ''anaokoteshwa'' award?
 
Kichwa cha hii habari kimekaa kizandiki.... walau kingekuwa "THE World Economic Forum (WEF) names Makamba one of its Young Global Leaders"
 
I love my country and some of my countrymen!!!!!

Mwanzo wa mabadiliko ya Taifa lolote ni pale watu wanapoanza kugeuza kila jiwe!!!!!
 
Hivi Bwana Makamba ka-achieve nini hadi sasa kinachoweza kuonekana?

Hili ni bomu linaloandaliwa!

1. Kampeni zake za uchaguzi zilidhaminiwa na makampuni ya madini
2. Alipelekwa kutambulishwa ikulu ya Marekani
3. Yuko anapambwa wakati hafanyi chochote cha maana

Kuwa makini sana na huyu dogo!
 

Hii habari ilikuwa ya uongo. Ni tatizo la waandishi wetu kupewa nini cha kuandika nao wanakurupuka. Ukiangalia kwenye list ya ygl inayosemwa huyo mtu hayumo kabisa! Labda kama walilificha jina lake au tuletewe hiyo list. Kwa kipi alichokifanya huyu mpuuzi anayeshindwa hata kusimamia ukusanyaji wa kodi kwenye makampuni ya simu wanakuja na hoja za kutaka kuchukua tena kutoka kwa wananchi. Urais wa kuota unawapa shida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…