Makali ya kufungiwa RFA

busiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2016
Posts
306
Reaction score
183
Jamani salamu zenu.

Naanza kwa kuipongeza serikali hii kwa namna inavyotafuta mapato kutoka vyanzo vya ndani,safi.

Pili ni kuhusu hali ilivyo tangu redio free Afrika ifungiwe kwa kutokulipa kodi kwa muda mrefu.Ndio kuna athali kubwa tu.
Mimi ni mwananchi niliyekuwa mlaji wa vipindi vyao.
Sasa baada ya hali hii kuwepo kiuhalisia hali ya upataji taarifa sio tena nzuri kama nitakavyoeleza hapa.

1.Sisi tulio vijijini(Geita vijijini)huwa hatuna namna ya kuchagua kama wenzetu wa mijini au mikoa mingine.

Ikumbukwe hii rfa ndio angalau ilikuwa inatupatia taarifa mbalimbali za nchi nzima kutokana na mpangilio wa vipindi vyake.

2.Sisemi kuwa hakuna radio station nyingine aanha!zipo,,,isipokuwa habari hatupati kwa wakati yaani katika masaa 24 ya siku.

3.Sasa ombi,kama uwezekano upo hawa radio one,magic fm efm msogeze huduma zenu nasi tuendelee kuwa duniani.

Radio zilizopo ni za kanda ambazo hazijakidhi mahitaji ya wasikikizaji.
Hizi za taifa zipo ila kama mjuavyo ni wachaguzi wa habari,yaani hawa habari nyingi ni kusifia serikari tu hata kama wanaujua uhalisia ulivyo wa maisha.

Wafanye mpango .Hali sio nzuri.Tunamisi magazeti asubuhi,vipindi vya habari angalau kila baada ya masaa matatu na hata elimu na burudani.
Mawingu wapo ila wao habari ni kwa masaa 12 kwa siku eti ni ya vijana.Sawa kabisa.

Naongeza tena radio one,magic fm na wengine mtuone huku.

Sent from my TECNO-Y3 using JamiiForums mobile app
 

Ndugu yangu ulichokisema ni sahihi nipo kyela one time kuna karedio ka wilaya huku Kyela fm wanategemea sana kupata magazeti ya asubuhi kupitia RFA imewapata hii pia. ila RFA WAKOME nao asee
 
BBC habar saa kumi na mbili, magazeti, matukio, habar za ujeruman saa saba, ujeruman saa kumi na mbili, bbc...... hivyo vipindi navipenda sana.... hata Diallo akipitisha bakur ntatoa pakubwa sana ili radio irud hewan...

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Usisubiri apitishe wewe nenda ofisi za sahara media peleka hela tu watampatia wale walinzi

May Allah bless Me and You
 
Nafikiri sasa ndio TRA walaumiwe walikuwa wapi siku zote mpaka mtu alimbikize deni kubwa hivyo? Ni aibu kwa nchi kumwachia mtu mwenye uwekezaji mkubwa hivyo mpaka deni likawa kubwa nanma hiyo,mfumo wetu wa kodi ni laini sana.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Reactions: SDG
Sasa si mjichange mumsaidie kulipa kodi.mbona mnatia aibu wa mikoani.?

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
[emoji116][emoji115]Malizeni UTATA


May Allah bless Me and You
 
Wamuombe bashite awasaidie maana walimpa airtime ya bure wkitegemea kuendelea kukwepa kodi eti kwa vile bashite ni mwana mpendwa wa mkulu
 
Tulioumia ni wengi Rfa ni radio iliyokuwa inachana mawimbi A mashariki na kati hata ukiwa porini huko kitu kinakamata tu ila muda si mrefu itarejea mazungumzo yanaendelea
 
Waende kwanza wakatubu mbele mola kwa kitendo chao cha kumkumbatia Bashite na Boss wake.
Wamepata laana ya kushabikia dhuluma.

Safi sana.
RFA ife kabisa.
 
Bora wewe mkuu upo huku JF, habari nyingi unaweza kuzipata huku..
wenzio hata JF hawaijui na RFA ndo kama hvyo imefungiwa...
But nakushauri download App za radio...So uwe unasikiliza kupitia smartphone yako utaenjoy saaaaaaanA..
 
Mtakuja tudai na madeni ya baba zetu, hivi hamna ukomo wa deni? Kama dingi alikwepa kodi mwaka 67 inakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…