Katibu wa Siasa na uenezi Ccm mkoa wa Tabora Iddi Moshi Mambo ametaja orodha ya majina ya watia nia wa udiwani wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Mambo, ameeleza kuwa majina hayo yamepitishwa na Chama cha mapinduzi CCM kwa ajili ya Wajumbe wa Chama hicho ngazi ya kata kuwapigia kura na kumchagua mmoja kuwa Mgombea wa Udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.