Hiyo ni kanuni ya pesa worldwide, kwa watu makini pesa inapotolewa au kutumika ni muhimu iambatane na uwekaji wa kumbukumbu ili iwe rahisi kuhakiki, kwa dunia ilivyo palipo na harufu ya pesa wapigaji nao huwa hawachezi mbali,kumbukumbu inasaidia kuhakiki kama kiasi kilichokusanywa hapo msibani kinaendana na kiasi halisi kilichochangwa na watu,vinginevyo wanaweza wakaja watu kumi kila mmoja amechanga elfu kumi lakini kwa kuwa hakuna record muhusika hapo mezani badala ya kuwasilisha laki moja akawasilisha sh. elfu kumi nyingine akatia mfukoni.
Hata hivyo huwa hakuna anayekulazimisha kuandika jina unapotoa kama hupendi kuandikwa,kwani wapo ambao imani zao zinawaelekeza mkono wa kulia unapotoa hata mkono wa kushoto hautakiwi kujua sembuse mwanadamu mwingine,so unaweza kuweka milioni yako bila kuandika na kama unajitambua hakuna wa kukulazimisha kuandika jina.